VIDEO:Kingunge Ngombale Mwiru aongea, ni kuhusu CHADEMA na Serikali - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 25, 2016

VIDEO:Kingunge Ngombale Mwiru aongea, ni kuhusu CHADEMA na Serikali


Aliyekuwa kada wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru  amewaomba  marais wastaafu, Rais Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa kuzungumza na Rais John Magufuli ili aitishe kikao kati ya Serikali na Chadema kwa ajili ya kusitisha maandamano yaliyopangwa kufanyika Septemba Mosi.

 Kingunge  ametoa kauli hii  Agosti 24,2016 nyumbani kwake jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari  wakati akiongelea  mvutano kati ya Chadema na Serikali unaoendelea kwa sasa.

Aidha ameongeza kuwa endapo Rais Magufuli atakubali kuitisha kikao watawageukia CHADEMA wasitishe mpango wao wa UKUTA kuepusha shari itakayoweza kutokea.

HAPA CHINI BOFYA KITUFE KUTAZAMA VIDEO ALICHOKIONGEA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad