Aidha Mhe. Kairuki alifafanua kuwa
data hizo chafu zilibainika wakati Wizara yake ikifanya uhakiki wa Watumishi
kujiridhisha na takwimu zilizotolewa kuhusu watumishi hewa na kubaini kuwa kuna
data chafu ambazo zinasababishwa na baadhi ya Watumishi kutokuwa na akaunti za
benki za kupitishia mishahra yao.
Pia baadhi ya nyaraka za Watumishi
kutofautiana majina na majina halisi wanayoyatumia kazini na yaliyopo katika
mfumo wa Taarifa za kiutumishi na mishahara (HCMIS).
Vilevile baadhi ya
Watumishi kuonekana kuwa tayari wamezidi umri wa miaka 60 ya kustaafu kwa
lazima lakini bado wanaonekana kuwa bado wapo kazini na wanalipwa mishara ya
Serikali.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa
Kagera, Mhe. Kijuu (Pichani Kulia) akitoa taarifa ya Mkoa kwa Mhe. Kairuki alisema kuwa Mkoa wa
Kagera una Watumishi 19, 982 aidha, katika zoezi la kuhakiki Watumishi hewa
Mkoa ulibaini watumishi hewa 274 waliolipwa kiasi cha shilingi bilioni
1,153,690,895.63 na fedha zilizorejeshwa ni shilingi Milioni 103, 725,731.23
sawa na asilimia 8.8%
Vile vile Mhe. Kijuu alimweleza
Waziri Kairuki kuwa Mkoa unakabiliwa na tatizo la baadhi ya nafasi za watendaji
kukaimiwa ambapo nafasi hizo ni 59, Jambo ambalo linasababisha baadhi ya
maamuzi katika ngazi mbalimbali kutotolewa kwa wakati na kwa usahihi kutokana
na Makaimu hao kutokuwa na madara kamili.
|
No comments:
Post a Comment