Tazama Matokeo yote ya VPL 2016/2017 huku Yanga SC ikianza Vyema kutetea Ubingwa wao. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 28, 2016

Tazama Matokeo yote ya VPL 2016/2017 huku Yanga SC ikianza Vyema kutetea Ubingwa wao.

Pichani juu ni Shabiki wa wakimataifa akijiandaa ki Afya kabla ya mtanange dhidi ya African Lyon. 

Mabingwa Watetezi wa Ligi kuu Soka Vodacom Tanzania bara, Yanga SC  wameanza Ligi Kuu  Msimu mpya wa 2016/2017 kwa mwendo kasi baada ya kushinda 3-0 dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Leo Agosti 28,2016.

Bao za Yanga SC zilifungwa na Deus David Kaseke katika Kipindi cha Kwanza na Simon Msuva na Juma Mahadhi kutikisa Kipindi cha Pili.

Nako huko Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, kwenye Mechi nyingine ya VPL, Wenyeji Toto Africans wamebwagwa na Mbeya City 1-0 kwa Bao la Mchezaji wao zamani Haruna Shamte.

VPL itaendelea tena Jumatano kwa Mabingwa Yanga SC kucheza na JKT Ruvu ndani ya Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Hapo jana Agosti 27,2016 - Simba SC alibanwa 0-0 na JKT Ruvu huko Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakati huko Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam, Azam FC ikiinyuka Majimaji 3-0.

Huko Manungu, Morogoro, Mtibwa Sugar waliifunga Ndanda FC 2-1wakati huko Sokoine, Mbeya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting zikitoka 1-1 na kule Kirumba Mwanza Mbao FC kupigwa 1-0 na Mwadui FC.

VPL 2016/2017-Ratiba

Jumatano Agosti 31,2016.

Yanga v JKT Ruvu   

Jumamosi Septemba 3,2016.

Mbao FC v Mbeya City

Jumatano Septemba 7,2016.

Simba v Ruvu Shooting  
  
Ndanda FC v Yanga

Tanzania Prisons v Azam FC    

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad