DED Ngara ashuhudia Ngara Stars wakiifunga Benaco FC ,Ligi Taifa daraja la nne wilaya ya Ngara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, August 28, 2016

DED Ngara ashuhudia Ngara Stars wakiifunga Benaco FC ,Ligi Taifa daraja la nne wilaya ya Ngara.


Pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara mkoani Kagera Aidan J. Bahama akisalimiana na wachezaji wa Timu ya Ngara Stars wakati wa Mchezo wa Ligi Taifa daraja la nne wilaya ya Ngara dhidi ya Benaco leo 28/08/2016 na Ngara Stars kuifunga Benaco FC goli 1 – 0,goli lililofungwa dakika ya 83 na Abdul Rupia.

Kwa ushindi huo wa leo, Ngara Stars sasa wanaongoza ligi kwa alama 15 wakifuatiwa na Benaco FC waliobaki na alama 12 katika Msimamo.


Nao Red Stars walisafiri hadi Kihinga kucheza na wenyeji Kihinga FC na wenyeji kufanikiwa kuwafunga Red Stars bao 1-0, goli lililofungwa na mchezaji Boniface Massawe dakika 37 na kuwafanya Kihinga FC kufikisha alama 9 katika msimamo wa ligi wakiwa nafasi ya nne. 


Huko katika Uwanja wa shule ya msingi Murukulazo, wenyeji Pasuamwamba FC wamekubali kulizwa bao 2-0 na Timu ya Walimu FC. 


Magoli ya Walimu FC  yamefungwa yote mawili na Moses John katika dakika ya 38 na 83 na kuwafanya wakamate nafasi ya 3 wakiwa na alama 12.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad