Picha Uongozi na Watumishi Radio Kwizera FM wampokea kwa Kishindo Bi.Auleria Gabriel baada ya Kutwaa Tuzo ya Mwandishi Bora wa Masuala ya Jinsia. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 26, 2016

Picha Uongozi na Watumishi Radio Kwizera FM wampokea kwa Kishindo Bi.Auleria Gabriel baada ya Kutwaa Tuzo ya Mwandishi Bora wa Masuala ya Jinsia.



Pichani katika tabasamu Mkurugenzi wa Radio Kwizera FM ,Ngara,Kagera sambamba na Wafanyakazi wa kituo hicho wakiwa na Bango Picha la Ushindi wa Kishindo wa Bi.Auleria Gabriel ambapo usiku wa kuamkia Ijumaa Agosti 19, 2016 huko nchini Namibia alitwaa Tuzo ya Mwandishi Bora wa Masuala ya Jinsia kutoka Nchini Tanzania.

Mapozezi hayo yamefanyika Agosti 25,2016 mjini Ngara.



 Licha ya kuiwakilisha nchi ya Tanzania vizuri,Kituo chake cha kazi Redio Kwizera  FM/ Ngara Mkoani Kagera,pia  Auleria Gabriel  kaweka historia ya kuwa Mtanzania wa kwanza kutwaa tuzo hii ya kimataifa kwa waandishi wa habari.



Akizungumza katika Hafla fupi ya Kumpongeza Bi. Auleria Gabriel Jana Agosti 25,2016,baada ya kushinda tuzo hiyo ya mwaka katika Uandishi wa Habari za Kijinsia  katika mashindano yaliyofanyika  huko nchini Namibia, Mkurugenzi wa Redio Kwizera FM, Padre Damas Misanga amewataka wandishi wa habari wa Redio hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano ili kutengeneza vipindi vyenye ubora na kuleta mabadiliko katika jamii na taifa kwa ujumla.


Pia Padre Misanga amesema kuwa ushindi huo sio wa Redio kwizera pekee bali ni Tnzania nzima lakini npia na Afrika kwa yeye ndiye mwana mke pekee ambaye ameshinda tuzo hiyo katika Bara la Afrika.

 Bi.Auleria Gabriel aliwashukuru Wafanyakazi wenzake na Uongozi wa Radio Kwizera kwa ushirikiano wao waliompatia mpaka kupata Tuzo hiyo.



Pamoja na mambo mengi Uongozi wa Radio na Watumishi ulimzawadia zawadi ya Kompyuta Mpakato (LAPTOP) na Vitu mbalimbali ikiwemo Fedha taslimu.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad