Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wanahabari Ikulu
jijini Dar es Salaam.
Waziri Modi aliongeza
kuwa Serikali ya India itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika
masuala mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuongeza wigo wa biashara na
hatimaye kukuza uchumi wa nchi hizo.
Kwa upande wake, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli alisema Serikali India
imekua na ushirikiano mzuri na Tanzania hasa katika masuala ya maendeleo ambapo
imeweza kuwekeza nchini kiasi shilingi za Kimarekani dola bilioni 2.4 na
kuzalisha ajira 54,176.
Baadhi ya misaada
iliyotolewa na Serikali ya India ni pamoja na
mashine ya vipimo vya ugonjwa wa kansa katika hospitali ya Bugando,
itakayosaidia wakazi wa kanda ya ziwa na nchi nzima kwa ujumla pamoja na
kuongeza na kuimarisha ushirikiano kati ya Shirika la viwanda vidogo vigodo la
India kushirikiana na Tanzania katika kukuza viwanda vidogo na vya kati nchini.
Katika masuala ya
teknolojia ya habari na mawasiliano, Serikali hiyo imeahidi kuleta wataalamu
wao nchini Tanzania kwa lengo la kutengeneza program mbalimbali ili kuisaidia
Tanzania katika masuala ya ulinzi wa mitandao pamoja na kutengeneza namna bora
za ukusanyaji wa mapato ya nchi.
Katika masuala ya
viwanda, Serikali ya India imeahidi kuanzisha viwanda vya kutengeneza dawa za
binadamu zitakazotibu magonjwa mbalimbali ikiwemo malaria, figo na
kisukari, ikiwa ni pamoja na kutengeneza vifaa tiba vitakavyotumika katika
hospitali mbalimbali nchini kwa lengo la kupunguza gharama ya kununua vifaa
hivyo nje ya nchi.
|
No comments:
Post a Comment