Mshambuliaji Antoine
Griezmann kaifungia mabao yote mawili dakika za 57 na 61 Timu yake ya Taifa ya Ufaransa ilipo shinda magoli 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Ireland katika mchezo wa hatua ya 16 Bora
Euro 2016 jioni ya leo,June 26, 2016 kwenye Uwanja wa Parc Olympique Lyonnais
mjini Decines-Charpieu na Ufaransa kwenda Robo Fainali.
Ufaransa walisawazisha
Dakika ya 57 kupitia Antoine Griezmann na Dakika 4 baadae Griezmann akapiga Bao
la Pili.
Jamhuri ya Ireland
walipata pigo jingine Dakika ya 66 pale Shane Duffy alipopewa Kadi Nyekundu kwa
kumwangusha Griezmann aliekuwa akichanja mbuga kumwona Kipa.
Kwenye Robo Fainali, Ufaransa
watacheza na Mshindi kati ya Uingereza na Iceland.
Jamhuri ya Ireland
walianza vyema na kupata Penati Dakika ya Pili tu pale Kiungo wa France Paul
Pogba alipomwangusha Shane Long ndani ya boksi na Mwamuzi Nicola Rizzoli wa
Italy kutoa Penati iliyopigwa na Robbie Brady na kupiga Posti ya chini na
kutinga wavuni.
Usiku huu,Ujerumani
wanaongoza bao 3-0 dhidi ya Slovakia
huko Stade Pierre Mauroy, Lille na kisha baadae Hungary dhidi ya Belgium huko Stadium de
Toulouse Mjini Toulouse.
Raundi ya Mtoano ya
Timu 16 ya EURO 2016 itamalizika Jumatatu,June 27, 2016 kwa Mechi mbili , ya
kwanza ni kati ya Italia dhidi ya Mabingwa Watetezi Hispania itakayochezwa
Stade de France, Paris wakati ya mwisho ipo Mjini Nice kati ya Uingereza na
Iceland.
Washindi wa Raundi hii
watatinga Robo Fainali ambazo Mechi zake zitaanza Alhamisi,June 30, 2016.
No comments:
Post a Comment