USALAMA BARABARANI:- Wakazi wa Isangijo Mwanza wamefunga barabara kwa zaidi ya saa 5 baada ya kugongwa kwa watoto 2. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, May 17, 2016

USALAMA BARABARANI:- Wakazi wa Isangijo Mwanza wamefunga barabara kwa zaidi ya saa 5 baada ya kugongwa kwa watoto 2.

Mamia ya wakazi wa kijiji cha Isangijo, kata ya Bukandwe wilayani Magu mkoani Mwanza Jana,May 16, 2016 ,Majira ya asubuhi wameifunga kwa mawe barabara kuu ya Mwanza – Musoma kwa zaidi ya saa tano baada ya watoto wawili wa shule ya msingi Isangijo kugongwa na daladala katika eneo hilo na kusababisha kifo cha mtoto mmoja wakati walipokuwa wakivuka barabara kuelekea shuleni.

Mwanafunzi aliyefariki dunia kwa kugongwa na daladala yenye namba za usajili T.155 DFX inayofanya safari zake kati ya Magu na Buzuruga jijini Mwanza ametambuliwa kwa jina la Juma Barnabas mwenye umri wa miaka minane anayesoma chekechea mwaka wa pili, ambapo majeruhi amefahamika kwa jina la Magreth Hade mwanafunzi wa darasa la kwanza.

Abiria walioonja adha hiyo ya kukaa kwenye foleni kwa zaidi ya saa tano baada ya barabara hiyo kufungwa kwa mawe pamoja na vifusi vya mchanga kuanzia majira ya saa moja na nusu asubuhi na kushindwa kuendelea na safari zao.

Mwalimu wa shule ya msingi Isangijo, Agnes Malikita akizungumzia tukio la kugongwa kwa watoto hao,amesema  walikuwa wakivuka barabara kwenye alama za pundamilia.

Diwani wa kata ya Bukandwe,Mhe. Marco Minze amesema zaidi ya watoto kumi wamewahi kugongwa katika eneo hilo, hivyo amewataka madereva kuwa makini kwa kuzingatia taratibu na sheria za usalama barabarani pindi wanapofika eneo hilo ili kuepusha ajali.TAARIFA ZAIDI ...BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad