Walimu 35,411 nchini wataajiriwa
katika shule za msingi na sekondari katika mwaka wa fedha 2016/2017.
Watakaokaidi kwenda kuripoti katika
mikoa ya pembezoni, hawataajiriwa na serikali.
Hatua hiyo imeelezwa kwamba imetokana
na serikali kupokea maombi mengi ya kazi kwa walimu, ambao mwaka jana,2015
hawakuripoti katika vituo walivyopangiwa pembezoni mwa miji kwa kutegemea
kuajiriwa na shule binafsi, lakini hawakufanikiwa.
Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Mhe. Selemani Jaffo Pichani, alisema hayo alipokuwa akijibu
swali la nyongeza la Mbunge wa Mchinga, Mhe.Hamidu Bobali (CUF) aliyetaka kufahamu
serikali inafanya nini kwa walimu waliopangiwa kwenda mikoa ya pembezoni,
ikiwemo Lindi na kwingineko, lakini hawakuripoti.
Mhe.Jaffo alisema ni kweli kuna walimu
wengi ambao hawakuripoti katika mikoa ya pembezoni. Alisema si Lindi peke yake,
bali na mikoa mingine, ikiwemo Katavi na Kigoma.
Alisema kwa mwaka huu,2016, wataajiri
walimu 35,411, lakini ambaye hataripoti katika mikoa hiyo na kuishia mijini tu,
hawataajiriwa tena serikalini, kama wanavyoomba tena baada ya kukosa katika
shule binafsi.
|
No comments:
Post a Comment