Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi
linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukamatwa wakiwa wanatoa fedha benki
ya NMB tawi la Mpanda kiasi cha shilingi 3,680,000 wakiwa na kadi za ATM 19
mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi hizo. .
Kaimu Kamanda wa Polisi wa mkoa wa
Katavi, Damasi Nyanda amesema watuhumiwa hao watatu walikamatwa jana majira ya
saa tatu usiku katika Tawi la NMB Mpanda .
Watuhumiwa hao ambao majina yao
yamehifadhiwa kwa kuwa upelelezi bado unaendelea, wamekamatwa na askari wa
jeshi la polisi waliokuwa wakilinda Benki hiyo.
Nyanda ameeleza kuwa watumiwa
walikamatwa baada ya askari polisi kuwatilia mashaka kutokana na kuwaona wakiwa
wamekaa muda mrefu kwenye chumba cha mashine ya kutolea fedha .
Amesema baada ya kuwatilia mashaka
polisi waliingia ndani ya chumba hicho na kuwakuta watuhumiwa hao wakiwa
wanaendelea kutoa fedha katika mashine tatu zilizomo kwenye mashine za kutolea
fedha.
Kaimu Kamanda alieleza ndipo askari
polisi walipoamua kuwapekua watuhumiwa na waliwakuta wakiwa na kadi za ATM 19
mali za watu tofauti pamoja na namba za siri za kadi h izo na walikuwa tayari
wameishatoa kiasi cha fedha taslimu shilingi 3,680,000.
Amezitaja Namba za Kadi za ATM
walizokamatwa nazo watuhumiwa kuwa ni AC 61908000058,AC
61902403196,AC61902400417,AC61908000427,AC 61902240100,AC 61908000237, AC
61902400518 AC 61910000645, AC 61910004240,AC 61908000609 AC 61902403168.
Kaimu kamanda Nyanda amezitaja kadi
za ATM zingine zilizokamatwa kuwa ni zenye namba AC 61910000537,AC 61902402653,
AC 61910000250, Ac 61902400818, AC 61908000449,AC1902403219 AC 61910002329 na
AC 70408100131.
Amesema watuhumiwa wanatarajia
kufikishwa mahakamani baada ya uchunguzi wa tukio hilo kukamilika na bado
watuhumiwa wote watatu wanaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano
zaidi .
Kaimu kamanda ametoa wito kwa
wananchi kuacha tabia ya kutoa siri kwa watu za namba zao za siri za kadi
wanazozitumia kwenye ATM za benki .BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
|
Saturday, May 28, 2016
UHALIFU / SHERIA YETU:-Mbaroni Kwa Kukutwa Wakitoa Mamilioni Kwa ATM Za Watu 19 .
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment