Rais Magufuli akizindua
nembo ya shirikisho la viwanda nchini, Waziri Mwijage, Mkurugenzi Mtendaji wa
Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodger Tenga na Mwenyekiti wa CTI Samuel
Nyantahe.
|
Rais Magufuli akitembelea baadhi ya
mabanda ya bidhaa zinazotoka Viwandani.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alialikwa katika hafla ya
utoaji tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo,May
31, 2016, Jijini Dar es Salaam.
Rais Magufuli
amewahakikishia wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda kuwa serikali yake
itatoa ushirikiano wa kutosha kwa wenye viwanda na wenye nia ya kuanzisha
viwanda vipya ili kufanikisha nia yake ya kuzalisha ajira nyingi, kukuza uchumi
na kuiwezesha serikali kukusanya mapato zaidi.
Hizi ni
sentensi tano alizozizungumza Rais Magufuli kwenye hotuba yake….
'Nimekaa serikalini kwa miaka 20, kuwekeana
wivu Mtanzania akitaka kuwekeza kupo sana, tumeamini watu kutoka nje kuliko
sisi wenyewe' – JPM
'tuweke nguvu kubwa kwa wanachi kuwa na
viwanda, nataka niwathibitishie nawapenda wafanyabiashara wenye nia nzuri ya
kuanzisha viwanda'-JPM
'Aina ya viwanda tunavyolenga kwa kiwango
kikubwa ni vya uzalishaji ambavyo hutumia malighafi zinazopatikana kwa wingi
ndani ya nchi' -JPM
'Nataka Nchi ya Viwanda halafu pawepo mtu
anakwamisha ataondoka, nimezunguka nchi nzima nasema nataka nchi ya viwanda
sikuwa kichaa' -JPM
|
No comments:
Post a Comment