“Tulifuata taratibu zote zikiwepo
mamlaka husika za nchi kma bodi ya sukari, Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na
vyombo vyote vya ulinzi na usalama,” amesema Murtaza.
Akifafanua zaidi amesema kuwa sukari
hiyo ilikuwa njiani kuelekea nchini Uganda na vielelezo vyote vipo lakini
kutokana na uhaba wa sukari nchini, serikali iliagiza mzigo huo kubaki nchini
na kuingiza sokoni ili kumaliza tatizo hilo ambapo ulitakiwa kuanza kuingia
sokoni kati ya Mei, 12 na Mei, 13.
Aidha ameelezea kuwa ni jambo la
kawaida kuagiza sukari kutoka Dubai kwani hutumia siku 7 pekee kufika nchini
tofauti na sukari kutoka Brazil ambayo hutumia siku 50 hadi 60 ikiwa njiani
hadi kufika nchini.
“Wafanyabiashara wote wanaojua
biashara walioko karibu na Dubai hufanya hivyo na sisi sio wa kwanza kuagiza
sukari kutoka kwa wauzaji wa Dubai,” amesema Murtaza.
Pia Murtaza amewatoa hofu Watanzania
kuhusu uhaba wa sukari kwa kusema kuwa tayari sukari imeagizwa na ndani ya wiki
mbili kutakuwa na sukari ya uhakika nchini hivyo kuwataka kuondoa hofu
iliyokuwapo hapo awali.
|
No comments:
Post a Comment