KLABU UTAJIRI DUNIANI:-Ni Real Madrid ikitamba mbele ya Barcelona na Manchester United. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 12, 2016

KLABU UTAJIRI DUNIANI:-Ni Real Madrid ikitamba mbele ya Barcelona na Manchester United.

Klabu ya Real Madrid ndio Klabu Tajiri Duniani ikitamba mbele ya FC Barcelona na Manchester United kwa mujibu wa Forbes ambao ni Magwiji wa Taaluma ya Fedha Duniani.

Mapato makubwa ya fedha zinazotokana na mauzo ya haki za matangazo ya TV , mauzo jezi na mapato ya udhamini wa jezi, wadhamini na ushiriki wa Klabu Bingwa barani Ulaya umeendelea kuzipa uthamani mkubwa vilabu vya soka duniani.
Mapato ya Champions League msimu uliopita

Kwa mujibu wa Jarida la Kimarekani la Forbes, Thamani ya Real Madrid ni Dola Bilioni 3.645 na Mapato yao kwa Mwaka ni Dola 694 Milioni wakiizidi kidogo Barcelona.

UEFA imeongeza malipo katika Mashindano ya Klabu Bingwa Ulaya, kwa asilimia 50% kwa miaka 3 kuanzia msimu wa 2015-2016. 

Fainali ya mwaka huu,UEFA ,May 28,2016, itakayochezwa San Siro jijini Milan, Italia, baina ya vilabu vya Hispania, Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid , kila timu itapata kiasi cha $100 million.
Klabu 6 za Ligi Kuu Uingereza, zipo kwenye 10 Bora huku Manchester United wakiongoza na nyingine ni Arsenal, Manchester City, Chelsea, Liverpool na Tottenham. 

Vilabu 20 ambavyo vinaongoza kwa uthamani vina thamani ya wastani wa $1.44 billion, ongezeko la 24% kuliko ilivyokuwa miaka 20 iliyopita. Malipo makubwa ya dili za TV, kama mkataba wa miaka wa miaka 3 wenye thamani ya $7.9 billion baina ya English Premier League na Sky Sports na BTSport ambao unaanza msimu wa 2016 / 2017, na dili nyingine za udhamini wa jezi, mfano ukiwa mkataba wenye thamani ya $130m kwa mwaka baina ya Manchester United na Adidas.
Timu yenye thamani kubwa ya soka kwa mwaka wa nne mfululizo ni Real Madrid wakiwa na thamani ya $3.65 billion, ongezeko la 12% la thamani waliyokuwa nayo mwaka uliopita.


Wanaowafuatia ni FC Barcelona ambao wana thamani ya $3.55 billion, ongezeko la 12% la thamani kutoka msimu uliopita.  

Barcelona huenda wakawapita wapinzani wao kutokana na mkataba wa $400 million la utengenezaji upya uwanja wao wa Camp Nou, ambao unategemea kukamilika ndani ya miaka mitano.
Timu ya 3 kwa thamani kubwa ni Manchester United, klabu ambayo ipo kwenye soko la hisa. 

Forbes wanaitaja kuwa na thamani ya $3.32billion, ongezeko la asilimia 7 la thamani kutoka mwaka jana. Man United wametengeneza faida ya $190m kwa msimu wa 2014 - 2015, kwenye listi  hii Manchester United ndio timu iliyoingiza faida kubwa kwa upande wa soka lakini wapo nyuma ya  Dallas Cowboys ($270 million) na New England Patriots ($195 million) kiujumla.

FORBES – 10 Bora ya Klabu zenye Thamani Duniani $=Dola (£=Pauni):

1 Real Madrid - US$3.645 bn (£2.52billion)

2 Barcelona - $3.549bn (£2.46bn)

3 Manchester United - $3.317bn (£2.3bn)

4 Bayern Munich - $2.678bn (£1.85bn)

5 Arsenal - $2.017bn (£1.4bn)

6 Manchester City - $1.921bn (£1.33bn)

7 Chelsea - $1.661bn (£1.15bn)

8 Liverpool - $1.548bn (£1.07bn)

9 Juventus - $1.299bn (£900m)

10 Tottenham - $1.017bn (£704m)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad