WENYE FEDHA BORA DUNIANI:-Cristiano Ronaldo amfunika Lionel Messi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 12, 2016

WENYE FEDHA BORA DUNIANI:-Cristiano Ronaldo amfunika Lionel Messi.

Jarida la biashara la Marekani,Forbes limemtaja staa wa Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo kuwa mwanasoka aliyetengeneza pesa nyingi mwaka 2015 kuliko wanasoka wengine.

Jarida hilo limesema Ronaldo kwa mwaka 2015 ambae huichezea Real Madrid ya Spain, alivuna Dola Milioni 82 kwa Mwaka uliopita zikiwa Dola Milioni 53 kama Mshahara na Dola Milioni 29 Mapato yatokanoyo na Matangazo na Udhamini.

Forbes pia limethibitisha kuwa hivi sasa Ronaldo ndie Mwanamichezo anaelipwa vizuri kupita mwingine yeyote katika Michezo yote.

Ronaldo anafuatiwa na mchezaji wa Barcelona na Argentina, Lionel Messi alievuna Dola Milioni 77 zikiwa Mshahara ni Dola Milioni 51 na Matangazo na Udhamini Dola Milioni 26 na nafasi ya tatu ikishikwa na Zlatan Ibrahimovic ambaye aliingiza Pauni Milioni 25.6.
Kwa mujibu wa Forbes, kwa wanamichezo wote ambaye alimpita kutengeneza pesa nyingi 2015 ni Kobe Bryant ambaye aliingiza Pauni Milioni 470 lakini pia mwezi Aprili alitangaza kustaafu kucheza mpira wa kikapu.

Kwenye Listi hiyo ya Wachezaji wanaolipwa Mapato ya juu Nahodha wa Manchester United na Uingereza, Wayne Rooney, anakamata Nafasi ya 6 akiwa ndie wa kwanza wale Wachezaji wachezao Ligi kuu uingereza akivuna Jumla ya Dola Milioni 26.

FORBES – 20 BORA KWA WACHEZAJI WANAOLIPWA JUU.

1 Cristiano Ronaldo (Real Madrid): $82m

2 Lionel Messi (Barcelona): $77m (£53.3m)

3 Zlatan Ibrahimovic (Paris Saint-Germain): $37m

4 Neymar (Barcelona): $36m

5. Gareth Bale (Real Madrid) - $34m

6. Wayne Rooney (Manchester United) - $26m

7. Sergio Aguero (Manchester City) - $24m

8. Luis Suarez (Barcelona) - $23m

9. Eden Hazard (Chelsea) - $22m

10. Cesc Fabregas (Chelsea) - $21m

11. James Rodriguez (Real Madrid) - $21m

12. Yaya Toure (Manchester City) - $20m

13. Radamel Falcao (Chelsea) - $19m

14. Thiago Silva (Paris Saint-Germain) - $18m

15. Mesut Ozil (Arsenal) - $18m

16. Bastian Schweinsteiger (Manchester United) - $18m

17. Angel Di Maria (Paris Saint-Germain) - $18m

18. Robin van Persie (Fenerbahce) - $17m

19. David Silva (Manchester City) - $17m

20. Samir Nasri (Manchester City) - $15m

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad