MAFANIKIO SOKANI 2015/2016:-Yanga SC yakusanya Mataji yote ikiifunga Azam FC mabao 3-1. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 25, 2016

MAFANIKIO SOKANI 2015/2016:-Yanga SC yakusanya Mataji yote ikiifunga Azam FC mabao 3-1.

Yanga SC imehitimisha msimu wa 2015/2016 kwa kutwaa mataji yote ya nyumbani, baada ya kuifunga Azam FC mabao 3-1 na kutwaa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) jioni ya leo,May 25, 2016, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kwa ushindi huo, sasa Yanga SC ni mbabe asiyepingika wa soka ya Tanzania, baada ya awali kutwaa Ngao ya Jamii Agosti 22, mwaka jana,2015 waliposhinda kwa penalti 8-7 dhidi ya Azam FC pia baada ya sare ya 0-0 na mapema mwezi huu kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,2015/2016.

Katika mchezo wa leo uliochezeshwa na Israel Nkongo, hadi mapumziko, Yanga SC walikuwa mbele kwa bao 1-0, lililofungwa na mshambuliaji kutoka Burundi, Amissi Tambwe dakika ya tisa kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia, Juma Abdul.
Dakika ya pili tu baada ya kuanza kipindi cha pili, Tambwe tena akawafungia Yanga SC  bao la pili, safari hiyo akimalizia krosi ya winga Simon Msuva.

Mshambuliaji Didier Kavumbangu akaifunga timu yake ya zamani, Yanga SC dakika ya 48 akiujaza mpira nyavuni kwa kifua kumalizia krosi ya winga Ramadhani Singano ‘Messi’.

Kiungo Deus Kaseke akaifungia Yanga SC bao la tatu dakika ya 81 kwa shuti kali akimchambua kipa Aishi Manula baada ya kupata pasi ya Msuva.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad