MABINGWA WA SOKA MKOA:-Murusagamba FC na Wapinzani wao Kituo cha Singida. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, May 28, 2016

MABINGWA WA SOKA MKOA:-Murusagamba FC na Wapinzani wao Kituo cha Singida.

Mabingwa wa soka Mkoa wa Kagera,Murusagamba FC.

Mabingwa hao wako Kituo cha Singida na timu shiriki ni Veyula FC (Dodoma), Pepsi SC (Arusha), Kitayosce FC (Kilimanjaro), Stand FC (Tabora), Fire Stone (Manyara) na Tomato FC (Njombe) na toka Mashindano yaanze ,Murusagamba FC wamepoteza michezo miwili kwa kufungwa bao 1 – 0 kutoka kwa Fire Stone na Pepsi SC.

Ligi hiyo inayoshirikisha timu 27, imegawanywa katika makundi manne ambako bingwa katika kila kundi atapanda daraja hadi Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/17 ngazi ya taifa kabla ya kutafuta nafasi ya kucheza Ligi daraja la Kwanza msimu wa 2017/2018.
Mabingwa wa Soka wa Mkoa wa Manyara,Fire Stone.

Timu tano zitapanda daraja hadi Ligi Daraja la Pili ambako mbali ya washindi katika vituo vyote vinne, mshindwa bora katika vituo vya Njombe, Morogoro na Singida nayo itapanda daraja kwa kuangalia vigezo vya wingi wa pointi, wastani wa mabao, mabao kufunga na mabao ya kufungwa. Kituo cha Kagera hakijajumuishwa kwa kuwa kina timu shiriki sita.
Mabingwa wa Soka wa Mkoa wa Arusha, Pepsi SC.
Mabingwa wa Soka wa Mkoa wa Tabora,Stand FC.

Kituo cha Njombe ,Timu zinazoshiriki ni Mkali Stars ya Ruvuma, Mtwivila (Iringa), Sido FC (Mbeya), Jangwani FC ya Rukwa, Nyundo FC ya Katavi, Mawezi ya Morogoro na Zimamoto ya Ilala, Dar es Salaam.

Kituo cha Morogoro , timu zinazoshiriki ni Stend  FC ya Pwani, Mbuga FC (Mtwara), Namungo FC(Lindi), Muheza United ya Tanga, Stand Misuna FC ya Singida, Makumbusho ya Kinondoni na Sifa Politan SC ya Temeke, Dar es Salaam.

Kituo cha Kagera , timu shiriki ni Geita Town Council Fc (Geita), Gold Sports Academy (Mwanza), Kabela City (Shinyanga), Ambassador FC (Simiyu), Igwe FC (Mara) na Mashujaa (Kigoma).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad