MATOKEO / RATIBA EPL 2015/2016:-Kocha Rafa Benitez ameteremka daraja akiwa na Newcastle United. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, May 12, 2016

MATOKEO / RATIBA EPL 2015/2016:-Kocha Rafa Benitez ameteremka daraja akiwa na Newcastle United.

Timu tatu zilizoteremka Daraja kutoka Ligi Kuu Uingereza Msimu huu 2015/2016 hadi  Daraja la kwanza, sasa zimejulikana baada ya mechi zilizoisha Jana May 11, 2016.

Klabu ya Aston Villa ambayo iliishajulikana, imepata wa kwenda nao ambao ni Norwich City ambayo imefanikiwa kushinda kwa mabao  4 - 2 lakini ikashindwa kujiokoa na Newcastle United ambayo ushindi wa mabao 3- 0 ilioupata Sunderland kutoka kwa Everton, umewadondosha.

Hivyo Kocha Rafa Benitez mwenye rekodi ya kubeba kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Liverpool, sasa ameteremka daraja akiwa na Newcastle United ambayo alipewa aiokoe.

Matokeo Mechi za Jumatano Mei 11,2016.

Norwich 4 – 2 Watford   

Sunderland 3 – 0 Everton                 

Liverpool 1 – 1 Chelsea             

LIGI KUU UINGEREZA 2015/2016 -RATIBA.

Jumapili Mei 15,2016.

**Mechi za Mwisho za Ligi, zote kuanza Saa 11 Jioni

Arsenal v Aston Villa        

Chelsea v Leicester         

Everton v Norwich          

Man United v Bournemouth                 

Newcastle v Tottenham             

Southampton v Crystal Palace              

Stoke v West Ham           

Swansea v Man City        

Watford v Sunderland               

West Brom v Liverpool  

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad