Hotuba
ya Mhe.Godbless Lema, Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni katika Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi ilizuiliwa leo asubuhikusomwa Bungeni hadi ipitiweupya
na kamati ya kanuni.
Bunge
liliahirishwaleo,May 16, 2016, asubuhi
hadi saa 10 jioni baada ya kuzuia kusomwa kwa hotuba hiyo kwa madai kwamba, ina
maneno yanayohitajika kuondolewa ili ikidhi matakwa baada ya kupitiwa na Kamati
ya Kanuni.
Ndani
ya Hotuba ya Mhe.Lemakipo kipengelea
kinachoelezea sakata la makataba tata wa Kampuni ya Lugumi ambapo Kamati ya
Mambo ya Ndani ilielezwa suala hilo kutojadiliwa Bungeni kwa madai tayari
lilikuwa limeanza kuchunguzwa na Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Kipengele
kinachohusu mkataba wa Kampuni ya Lugumu kipo kwenye sehemu ya tano inayoeleza
Mikataba Tata ya Jeshi la Polisi.
Kwa
muda mrefu mkataba huo uliotolewa na Jeshi la Polisi nchini kwa Kampuni ya
Lugumi Enterprises Ltd wenye thamani ya Sh 37 bilioni umedaiwa kuwa na harufu
ya ufisadi.
Mwaka
2011, kampuni hiyo ilipewa zabuni ya kufunga mashine za alama za vidole katika
vituo vya polisi 108 nchini na kulipwa Sh 34 bilioni kati ya Sh 37 bilioni sawa
na asilimia 99 ya malipo yote.
Mambo
mengine yaliyosababisha hotuba hiyo izuiliwe niUuzwaji wa nyumba uliomtaja Rais John Magufuli moja kwa moja, Rushwa na
Bunge kutumika kuwalinda watuhumiwa , tabia ya Rais na Usalama wa nchi na
mwisho ni kuwataja viongozi wa juu wa serikali kwa maneno ya dhihaka.
No comments:
Post a Comment