Watuhumiwa wawili Zuberi Thabiti (30)
na Iddy Adamu (32) wanaodaiwa kushirikiana kufanikisha tukio la kumbaka na
kumdhalilisha binti wa miaka 21, mkulima (jina limehifadhiwa), mkazi wa Kata ya
Dakawa, wilayani Mvomero, mkoani Morogoro, wamekamatwa na kohojiwa na Jeshi la
Polisi mkoani humo.
Watuhumiwa hao wanadaiwa kufanya
tukio hilo la kinyama usiku wa Mei 4, mwaka huu,2016 katika nyumba ya kulala wageni
iitwayo Titii iliyoko Dakawa ambapo Zuberi ambaye ni dereva, mkazi wa Mbarali
Mbeya anadaiwa kumbaka binti huyo huku Iddy ambaye ni mkulima, mkazi wa
Makambako akirekodi picha za video kwa kutumia simu yake ya mkononi.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi,
baada ya kurekodi katika simu yake, baadaye Iddy alizituma picha hizo kwa mtu
aliyefahamika kwa jina la Rajabu Salehe (26), mkazi wa Dakawa ambaye naye
alizisambaza picha hizo katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwa watu
mbalimbali.
Taarifa ya polisi imeeleza kuwa,
chanzo cha tukio hilo ni kwamba, binti huyo alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na
Zuberi ambapo siku hiyo mtuhumiwa alimpigia simu binti huyo na kumwambia aende
katika nyumba hiyo ya wageni.
Taarifa hiyo ya polisi imezidi
kueleza kuwa, baada ya kufika katika chumba husika ndipo Iddy alipoingia kisha
kumtaka binti huyo afanye atakachomuelekeza huku akimshikia kisu ili asipige
kelele na baada ya kutekeleza ukatili huo (ubakaji), walimtaka asitoe siri hiyo
vinginevyo atauawa.
Aidha, baada ya tukio hilo kuripotiwa
kituo cha Polisi Dakawa Apliri 5, mwaka huu, polisi walianza uchunguzi mara
moja ambapo walifanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 11 wakiwemo Zuberi na
Iddy pamoja na walioshiriki kuzisambaza picha hizo za udhalilishaji ambao ni;
Rajabu Salehe (26), Saidi Athumani
(26), Musini Ngai (36), Saidi Mohamedi
(24), John Peter (24), Hassani Ramadhani (27), Ramadhani Ally (26), Lulu Peter
(38) na Magreth Njonjome (30), wote wakazi wa Dakawa ambapo kwa pamoja
wamefunguliwa shitaka la PICHA ZA UTUPU (P.O.N.O.GRAFIA) chini ya kifungu cha
14 (1) (a) cha sheria ya makosa ya mtandao.
Taarifa hiyo ya polisi pia imeeleza
kuwa jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine huku jeshi hilo
likitoa onyo kwa wananchi wote kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii
kwa kutoshiriki makosa ya uhalifu wa kimtandao kwani sheria itachukua mkondo
wake.
Katika hatua nyingine, Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu leo alikemea suala
hilo bungeni na kueleza masikitiko yake makubwa kwa watu hao kutekeleza unyama
huo na kusisitiza kuwa watuhumiwa hao wafikishwe mahakamani haraka.
|
No comments:
Post a Comment