MATOKEO / RATIBA VPL 2015/2016:-Simba SC na Azam FC zashinda mechi za leo May 15, 2016..Nafasi ya Pili bado Kazi tuu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, May 15, 2016

MATOKEO / RATIBA VPL 2015/2016:-Simba SC na Azam FC zashinda mechi za leo May 15, 2016..Nafasi ya Pili bado Kazi tuu.

Basi la Klabu ya Simba SC..

Wekundu wa Msimbazi Simba SC imeibuka na ushindi wa kwanza baada ya mechi nne za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,msimu huu 2015/2016 kufuatia kuichapa bao 1-0 Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro,Leo Jumapili May 15, 2016.

Shujaa wa Simba SC ni kiungo Abdi Hassan Banda aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 70 kwa kichwa akimalizia krosi nzuri ya beki wa kushoto, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

Tangu iifunge 2-0 Coastal Union mjini Tanga, Simba SC haijashinda mechi nyingine ya Ligi Kuu hadi iliposhinda tena leo.
Kikosi cha Simba SC.

Ushindi huo unaifanya Simba SC ifikishe pointi 62 baada ya kucheza mechi 29 ikiendelea kukamata nafasi ya tatu nyuma ya Azam FC yenye pointi 63 na mabingwa Yanga SC, wenye pointi 72.

Mchezo mwingine wa ligi hiyo leo,May 15, 2016, Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji African Sports Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Mabao ya Azam FC yamefungwa na mshambuliaji Mkenya Allan Wanga dakika ya 10 na beki Erasto Nyoni dakika ya 74, wakati la Sports limefungwa na Omary Ibrahim dakika ya 11.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad