|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli na mkewe Mama Janeth
Magufuli wakishuhudia wenyeji wao Rais
Paul Kagame na Mama Janeth Kagame pamoja na binti yao wakiweka shada la maua
katika viwanja vya Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbali mjijini Kigali, Rwanda, leo
April 07,2016.
Mkuu wa kitengo cha Rwanda cha
kupambana na mauaji ya kimbari Dkt Jean Damascene Bizimana, akihutubu wakati wa
maadhimisho mafupi ya kukumbuka mauaji hayo, amezihimiza nchi za Afrika
Mashariki kubuni sheria za kufwatilia na kuwadhibiti watu wanaoeneza itikadi za
mauaji ya kimbari.
Amesema nchi za Burundi na Jamuhuri
ya Kidemokrasia ya Congo zilitoa hifadhi na kushirikiana na wapiganaji wa kundi
la FDLR wanaotuhumiwa kutekeleza mauaji hayo.
Amesema Rwanda imefurahishwa sana na
taifa la Ujerumani kwa kuwakamata na kuwahukumu vinara wa kundi hilo wanaoishi
nchini Ujerumani kutokana na mchango wao katika mauaji yanayotekelezwa na kundi
hilo nchini Congo.
Viongozi hao wa FDLR ni Ignace
Murwanashyaka aliyehukumiwa miaka 13 jela na Straton Musoni aliyehukumiwa miaka
8 jela.
Mwandishi wa BBC aliyeko Rwanda Yves
Bucyana anasema kutakuwa na wiki nzima ya maombolezo kukumbuka waliouawa wakati
wa mauaji hayo.
Shughuli za michezo na burudani
zimepigwa marufuku huku bendera zikipepea nusu mlingoti.
Dkt Magufuli amekuwa kwenye ziara
rasmi ya siku mbili nchini Rwanda, ziara yake ya kwanza nje ya nchi tangu
kuingia madarakani Novemba mwaka jana,2014.
Ameondoka Kigali na kurejea Dar es
Salaam.
Source:-BBC Swahili.
|
No comments:
Post a Comment