ORODHA YA FIFA YA BORA DUNIANI:-Tanzania na Kenya zashuka . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 07, 2016

ORODHA YA FIFA YA BORA DUNIANI:-Tanzania na Kenya zashuka .

Wachezaji wa Taifa Stars ya Tanzania.

Nchi ya Tanzania,Kupitia timu yake ya Taifa -Taifa Stars imeshuka nafasi 5 kwenye orodha ya viwango vya ubora wa soka ya FIFA iliyotolewa leo,April 07,2016 wakati Kenya imeshuka nafasi 12 .

Tanzania inakamata nafasi ya  130 huku Kenya kwa sasa wako nafasi ya 115.

Tanzania hawajahesabiwa mechi yoyote ya karibuni. Walishinda 1-0 dhidi ya Chad mechi ya kwanza ugenini lakini Chad wakajiondoa na hawakushiriki mechi ya marudiano jijini Dar es Salaam. 

CAF ilifuta matokeo hayo dhidi ya Chad katika kundi G.
Mchezaji wa Harambee Stars kwenye mechi ya awali.

Harambee Stars wameshuka baada ya kushindwa mechi mbili za kufuzu kwa Kombe la Mataifa Bingwa Afrika na Guinea Bissau.

Taifa hilo la Afrika Magharibi limepanda hatua 45 hadi nambari 102.

Guinea Bissau waliichapa Kenya 1-0 mechi ya kwanza tarehe 23 Machi na kwenye mechi ya marudiano wakashinda tena 1-0 jijini Nairobi.

Miongoni mwa mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uganda inaongoza ikiwa nafasi ya 72, Rwanda inafuata nafasi ya 87, Kenya nafasi ya 115, Burundi nafasi ya 122, Tanzania ya 130 na Sudan Kusini nafasi ya 155.

Orodha ya mataifa kumi bora Afrika ni kama ifuatavyo:

    Algeria

    Ivory Coast

    Ghana

    Senegal

    Misri

    Cape Verde

    Tunisia

    Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

    Guinea

    Congo

Duniani, orodha ya kumi bora ni kama ifuatavyo:

    Argentina

    Ubelgiji

    Chile

    Colombia

    Ujerumani

    Uhispania

    Brazil

    Ureno

    Uruguay

    England

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad