TASWIRA PICHA:-DC Ngara na Wananchi wa Kata ya Kasulo kutekeleza Agizo la Waziri Mkuu wa Tanzania. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 07, 2016

TASWIRA PICHA:-DC Ngara na Wananchi wa Kata ya Kasulo kutekeleza Agizo la Waziri Mkuu wa Tanzania.


Wananchi wa Kijiji cha Rwakalemela kata ya Kasulo wilayani Ngara mkoani Kagera wakiwa kwenye mkutano wa kijiji leo April 07, 2016 wakipokea taarifa ya mapato na matumizi.


Mkutano huo umefanyika Kufuatia  kutekeleza Agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe Kasimu Majaliwa  akiwa ziarani wilayani Ngara alipowataka Viongozi wa wilaya hiyo kuhakikisha Vijiji vya kata ya Kasulo vinapewa Sh milioni 8  za msitu wa Rumasi, jambo ambalo limeleta mzozo leo na kuahidiwa kuwa mchakato bado unaendelea.


Katika hatua nyingine,Mkuu wa wilaya ya Ngara,mkoani Kagera Bi.Honoratha Chitanda (Pichani mwenye Kipaza Sauti ) amewataka Wananchi wa kata ya Kasulo,wilayani humo kujihadhari na maambukizi ya Ugonjwa wa Ukimwi kwa kuwadhibiti vijana wanaojitembeza kwa madereva wanaoegesha magari kwenye mji wa Benako na hatimaye kupunguza nguvu kazi ya Taifa.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Rwakalemela  wilayani Ngara mkoani Kagera, Bw.Braithon Kemikimba akifafanua  hatua zinazoendelea za kupata asilimia 10 za mapato ya kijiji  hicho kutoka Halmashauri ya wilaya hiyo, katika kutekeleza agizo la Waziri mkuu Kasimu Kasimu Majaliwa wakati wa ziara yake mkoani Kagera.

Picha na Shaaban Ndyamukama.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad