Fastjet kwa hivi sasa inafanya safari mbili za kwenda
na kurudi kati ya miji hiyo kila siku
ndani ya wiki na hivyo kufanya jumla ya safari zake kwa wiki kati ya Uwanja
wa Kimataifa wa Dar es Salaam na Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta kuwa ni 28.
Mtiririko mpya wa safari unawapatia wateja
huduma sahihi mapema nyakati za asubuhi na
jioni na matokeo ya ratiba hiyo ni kuwepo kwa takribani viti 19,000 kila mwezi kwenye safari hizo
kati ya majiji hayo mawili na hali kadhalika kuwapatia wateja mbadala sahihi wa kusafiri kwa nauli
wanayoimudu.
Nauli za fastjet kimsingi ni za chini
ikilinganishwa na tozo za mashirika mengine ambayo kwa sasa yanafanya safari
zake kati ya Kenya na Tanzania.
Nauli
kutoka Tanzania kwenda Kenya
zinaanzia shilingi 176,000 kwa safari moja, bila kodi ambayo ni shilingi
107,800 kwa kuondokea Tanzania na dola
40 kwa kuondokea Kenya, na hivyo fastjet kuwashauri abiria kukata tiketi zao
mapema kabla ya siku ya kuanza safari ili kutumia fursa hiyo ili kufaidi na
nauli ya chini.
Nauli kutoka Kenya zinaanzia dola za Marekani
120 kwa safari moja zikijumuishwa kodi za serikali ambayo ni dola 40 kwa
kuondokea Kenya.
Matokeo ya safari hizi kati ya
Nairobi na Dar es Salaam yamekuwa ni makubwa kutokana na ukweli
unaojidhihirisha kwamba nauli kwenye mashirika shindani yanayofanya safari kati
ya nchi hizi mbili zimeshuka kwa kiwango cha asilimia 40 tangu fastjet ianzishe
safari zake.
Fastjet inasisitiza kwamba kupunguza mtiririko wa safari kwenye njia
kati ya Nairobi na Kilimanjaro kunafungua fursa
ya kuongeza uwezo zaidi kwa njia zilizopo kwenye ukanda wa Afrika
Mashariki na hali kadhalika kuwepo uwezekano wa kufungua njia nyingine mpya
siku za karibuni.
|
No comments:
Post a Comment