Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa akitazama ngoma baada ya kuwali kwenye uwanja wa ndege wa
Bukoba kwa ziara ya kikazi mkoa wa Kagera Machi 13, 2016. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu).
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amesema Serikali imeanza kukusanya fedha kwa ajili ya kununua
meli mpya kwa ajili ya usafirishaji wa abiria na mizigo kwenye Ziwa Victoria.
“Rais John
Pombe Magufuli kasema ununuzi wa meli mpya uko pale pale. Tutanunua meli ya
kusafirisha abiria katika Ziwa Victoria kama ambavyo aliahidi wakati wa
kampeni,” alisema huku akishangiliwa.
Ametoa kauli
hiyo leo mchana (Jumapili, Machi 13, 2016) wakati akitoa maelekezo baada ya
kupokea taarifa ya mkoa wa Kagera ambako amewasili leo kwa ziara ya siku tatu
kwa ajili ya kukagua masuala ya wakimbizi pamoja na mwenendo wa ranchi zilizo
chini ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na jinsi zinavyotumika.
Mbali ya
ununuzi wa meli hiyo, Waziri Mkuu alisema Serikali pia imejipanga kununua ndege
mbili ili kuimarisha usafiri wa anga hapa nchini. “Tuna dhamira ya kununua
ndege walau mbili kwa ajili ya shirika letu la ndege la ATC.
Tumelazimika
kuwaomba Watanzania wenzetu warudi nyumbani ili kusaidia kuendesha shirika
letu,” alisema.
Waziri Mkuu
alisema suala hilo limeshafika mbali na utekelezaji wake hautachukua muda mrefu
kuanzia sasa.
Alitumia fursa
hiyo kuwaarifu wana Kagera kwamba hivi karibuni Serikali itaanza mradi wa
kujenga bomba la kusafirisha mafuta ambalo litapita kwenye mkoa huo na hivyo
ktoa ajira kwa wakazi wake.
“Bomba litaanzia Tanga, kupitia Kilimanjaro,
Arusha, Manyara, Simiyu, Geita, Kagera hadi Uganda. Na humu njiani litakuwa na
vituo vya kusukumia mafuta, kwa hiyo tuna uhakika wa kupata ajira kwa ajili ya
watu wetu,” alisema.
|
No comments:
Post a Comment