HAPA KAZI TU:-Waziri Mkuu wa Tanzania awasili Kagera kwa ziara ya kikazi...Ngara ni March 15,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, March 13, 2016

HAPA KAZI TU:-Waziri Mkuu wa Tanzania awasili Kagera kwa ziara ya kikazi...Ngara ni March 15,2016.


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma baada ya kuwali kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba kwa ziara ya kikazi mkoa wa Kagera Machi 13, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera, Bi Honoratha Chitanda amesema Waziri  Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Bw Majaliwa Kassim Majaliwa , atapokelewa March 15, mwaka huu 2016.



Amesema akiwa wilayani humo,Waziri Mkuu Majaliwa,kwa kutembelea kituo cha kupokelea Wakimbizi cha Lumasi,kilichopo Kata ya Kasulo/Benaco ,kutembelea kituo cha Kufulia Umeme kilichopo eneo la Nakatunga,mjini Ngara ,kuangalia maendeleo ya Mradi huo,Kuweka jiwe la Msingi sambamba na kuongea na Wananchi.


Amesema wilaya ya Ngara imejipanga kikamilifu kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa kwa wageni wote watakaofika kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera ikiwemo malazi na chakula.


 Bi Chitanda amewaomba wananchi wa wilaya hiyo kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumsikiliza waziri Majaliwa ili wafahamu nini alichokipanga kukifanya kwa ajili ya kuendeleza wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad