‘’Wekundu wa
Msimbazi’’Simba SC imeendelea kutamba kwenye Ligi Kuu soka ya Vodacom Tanzania bara msimu huu
2015/2016 baada ya kuinyamazisha Tanzania Prisons ya Mbeya bao 1- 0 kwenye
mchezo wa raundi ya pili ya Ligi uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa,Jioni ya Leo
March 13, 2016.
Ushindi huo
ni kisasi kwa Simba SC baada ya kufungwa 1-0 na Prisons katika mchezo wa kwanza wa
Ligi Kuu msimu huu Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Bao pekee
lililoipa Pointi 3, Simba SC limewekwa wavuni dakika ya 86 na kiungo Awadh Juma
kwa shuti kali akiwa nje ya box la 18 na kupeleka shangwe mtaa wa Msimbazi,
Kariakoo.
Matokeo hayo yanaifanya sasa, Simba SC wameshinda
mchezo wa tatu mfululizo baada ya kufungwa na Yanga SC bao 2- 0.
Wekundu wa
Msimbazi sasa wanafikisha pointi 54 baada ya kucheza mechi 23 wakiwazidi pointi
nne, mabingwa watetezi, Yanga SC walio nafasi ya pili, lakini wamecheza mechi
pungufu, 21. Azam FC yenye pointi 47 za mechi 20 ni ya tatu.
Mchezo
mwingine wa Ligi Kuu leo, Mgambo JKT imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na
Mwadui FC ya Shinyanga Uwanja wa Mkwakwani, Tanga, wakati jana March 12,2016 , Mtibwa Sugar
imeifunga 2-1 JKT Ruvu Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro.
|
No comments:
Post a Comment