|
Afisa Ardhi wa Wilaya ya Ngara, Betty Munuo wa Pili kushoto
na Mwenyekiti wa kijiji cha Rwakalaman,
Brighton Kemkimba (kulia) wakimsikiliza Waziri Mkuu wakati
alipozunguma katika kijiji cha Kasulo
wilayani Ngara machi 16, 2016.
Bi. Munuo ambaye amehamishiwa wilaya
hiyo Agosti, mwaka jana, alisema
aliyakuta malalamiko hayo na amefanya uchambuzi wa majina ya wamiliki wote wa
mashamba na walikuwa wanapanga kuwapatia notisi ili wajieleze.
Katika orodha yake, Bi. Munuo alitaja
wamiliki 18 wa mashamba makubwa lakini kati yao ni wamiliki saba tu ambao
mashamba yao yana hati lakini matatu ndiyo yameendelezwa na manne
hayajaendelezwa.
Mashamba yaliyoendelezwa yanatumika
kwa kilimo, ufugaji na shule. Nayo
yanamilikiwa na Dayosisi ya Rulenge (shamba na. 606 lenye ekari 161 liko
Mbuba); Dario Zakaria (shamba na. 639 lenye ekari 282 liko Nyakariba) na
Masista wa Mt. Fransisco (shamba na. 234 lenye ekari 759 liko Kasulo).
Mashamba manne yenye hati lakini
yametelekezwa ambayo yote yako kijiji cha Rwakalemera ni ya Abdallah Sadala na.
235 lenye ekari 521; Mahsen Saidi shamba na. 333 lenye ekari 458; Mshengezi
Nyambele shamba na. 746 lenye ekari 388 na
Mushengezi Nyambele shamba na. 745 lenye ekari 497.
Akitangaza uamuzi wake, Waziri Mkuu
aliwataja wamiliki wa mashamba yasiyo na hati kuwa ni Bw. Joseph Rugumyamheto
mwenye shamba na. 527 (ekari 505 liko Rwakalemera); Bw. Nicolaus Kidenke shamba
halina namba na ukubwa wake haujulikani; Bw. Gwasa Angas Sababili shamba na.
714 (ekari 236 liko Kasharazi); na Bw.
Makumi Adili Rufyega (ekari 500 liko Rwakalemera).
Wamiliki wengine ambao mashamba yao
yapo kijiji cha Rwakalemera ni Paulo Shikiri ekari 250; Frank Mukama Derila
ekari 750; Godfrey Kitanga ekari 800; Philemon Mpanju ekari 200; Issa Sama
ekari 500; Hekizayo Mtalitinya ekari 225 na Joel Nkinga ekari 1,250.
Waziri Mkuu aliagiza ifanyike sensa
ili kubaini kama wamiliki wa mashamba hayo yote ni Watanzania au la. "Haya
yenye hati nataka yafanyike mapitio ya hati zao na kubainisha ni namna gani
walipatiwa hati hizo. Nataka taarifa inifikie ofisini kwangu Dar es Salaam
ifikapo tarehe 20 Machi, 2016," alisema.
Ili kukamilisha kazi hiyo, Waziri
Mkuu ameagiza kurejeshwa mara moja kwa aliyekuwa Afisa Ardhi wa Wilaya hiyo,
Bw. Enock Mponzi ambaye amehamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ili aje
asaidie uchunguzi wa ugawaji wa maeneo hayo.
Alimtaka Mwenyekiti wa kijiji cha
Rwakalemera, Bw. Brighton Kemikimba aitishe mkutano wa kijiji kabla ya tarehe
31 Machi 2016 na abainishe mashamba yote makubwa ambayo yanazidi ekari 50. Pia
afuatilie kama yana kibali cha Baraza la Madiwani.
Wakati huohuo, Waziri
Mkuu ameagiza kusimamishwa kazi kwa
aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara, Bw. Colnel Ngudungi na
kutaka arejeshwe wilayani humo kujibu tuhuma za kuhusika na upotevu wa fedha za
mauzo ya mbao kutoka kwenye msitu wa Rumasi, wilayani humo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa
Kagera, Bw. Adam Swai ameagizwa
kumwandikia barua Katibu Tawala wa Mkoa
wa Shinyanga ili atekeleze maagizo hayo na Bw. Ngudungi arejeshwe Ngara kujibu
tuhuma hizo. Bw. Ngudungi alihamishwa
kwenda Sekretarieti ya Mkoa wa Shinyanga, Agosti 2015.
Akiwa njiani kuelekea Ngara jana
mchana (Machi 15, 2016), waziri Mkuu alisimamishwa katika kijiji cha
Rwakalemera na wananchi wenye mabango wakiomba kurejeshewa ardhi ya kijiji huku
baadhi yao wakidai wanatishiwa na bunduki pindi wakisogelea mashamba hayo
makubwa.
Pia walidai kuuzwa kwa msitu wa
Rumasi na mapato kutojulikana yalipokwenda huku wakidai kuwa kijiji chao
hakipati mapato yoyote kutokana na minada ya ng’ombe inayofayika kijijini hapo
wakati sharia inataka asilimia 20 ya mapato ibakizwe kijijini.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, MACHI 16, 2016.
|
No comments:
Post a Comment