MATOKEO / RATIBA VPL 2015/2016:-Azam FC Yaweka hai mbio za Ubingwa wakizifukuza Vinara Simba SC na Yanga SC. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 17, 2016

MATOKEO / RATIBA VPL 2015/2016:-Azam FC Yaweka hai mbio za Ubingwa wakizifukuza Vinara Simba SC na Yanga SC.

Kipa wa Stand United, Frank Muwange  akiokoa moja ya hatari langoni mwake. Ambapo goli la Dakika ya 62 la Shomari Kapombe likawapa ushindi wa Bao 1-0 Azam FC walipocheza Mechi ya Ligi Kuu Vodacom, na Stand United Jana March 16, 2016 hii huko Azam Complex, Chamazi , Jijini Dar es Salaam na kuweka hai mbio zao za Ubingwa wakizifukuza Vinara Simba SC na Yanga SC.
Beki wa Stand United, Assouman N’guessan (kulia) akichuana na mshambuliaji wa Azam FC, Allan Wanga.

Hivi sasa VPL inaongozwa na Simba SC waliocheza Mechi 23 na wana Pointi 54, wakifuata Yanga SC wenye Pointi 50 kwa Mechi 21 na ya 3 ni Azam FC yenye Pointi 50 kwa Mechi 21 ambao wana uhafifu wa Magoli ukilinganisha na Yanga SC.
Ligi hii itaendelea Ijumaa kwa Mechi 1 kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar.

LIGI KUU VODACOM  VPL 2015/2016 – RATIBA.                     

Ijumaa Machi 18,2016.

Kagera Sugar v Mtibwa Sugar

Jumamosi Machi 19,2016.

Coastal Union v Simba

Majimaji v Mbeya City

Stand United v Ndanda

Jumapili Machi 20,2016.

African Sports v Tanzania Prisons

Jumatatu Machi 21,2016.

Mgambo JKT v Toto Africans

Alhamisi Machi 24,2016.

African Sports v Toto African

Mashabiki Stand United wakifutilia pambano  hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad