Waziri Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa awasili Mkoani Kagera
kwa ziara ya siku tatu kuanzia Machi 13
hadi 15, 2016 katika Manispaa ya Bukoba, Wilaya za Missenyi, Karagwe na Ngara.
Akitaja
malengo ya ziara yake mara baada ya kuwasili Mkoani Kagera alisema lengo kuu la
ziara yake ni kwenda katika ranchi za Missenyi
na Kitengule Wilayani Karagwe ili kujionea zinafanyaje kazi na kuona
jinsi ya kutatua changamoto mbalimbali
ili kuwepo ufugaji bora na kuondoa migogoro ya wafugaji na wakulima.
Lengo la
pili la ziara ya Mhe. Majaliwa alisema ni kutembelea Gereza la Mwisa Wilayani Karagwe na Ngara ili
kujionea maendeleo ya wakimbizi wafungwa wanajeshi walioletwa na Serikali
katika Magereza hayo ili kuwafunza wawe raia wema mara baada ya kubainika katika kambi ya
wakimbizi iliyopo mkoani Kigoma wakiendesha mafunzo ya kijeshi kwa wenzao
kambini.
Mara baada
ya kusomewa taarifa ya Mkoa wa Kagera na Mkuu wa Mkoa John Mongella Waziri Mkuu
Mhe. Kassim Majaliwa alitoa rai kwa wananchi na viongozi wa Mkoa kuhakikisha
wanaulinda Mkoa ili usiingiliwe na wahamiaji haramu kutoka nchi jirani ikiwa ni
pamoja na ardhi kutouzwa kiholela kwa wageni kutoka nje.
Aidha,
Waziri Mkuu Mhe, Majaliwa aliwaonya Wakuu wa Wilaya za Missenyi, Kyerwa na
Ngara kuhakikisha wanaziba mianya ya udhaifu ilipo kwa kuingiza mifugo na
uuzwaji wa ardhi holela katika Wilaya hizo huku wao wakiwepo kama vingozi wa
Serikali, alisema wanatakiwa kuchukua hatua haraka sana kuziba mapungufu hayo.
Pia alitoa
agizo kwa Afisa Uhamiaji wa Mkoa na Maafisa Uhamiaji wa Wilaya kuhakikisha
watekeleza majukumu yao ipasavyo na kuacha mara moja tabia ya kutoa vibali hovyo
vya watu kutoka nchi jiarani na kuhamia katika Mkoa wa Kagera na kuingiza
mifugo pamoja na kuhozi ardhi ya wazawa.
Vilevile
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alisistiza juu ya ukusanyaji wa kodi ili
Serikali iweze kuwaletea wananchi maendeleo yao. Alihoji juu ya utoroshwaji wa
Madini ya bati Wilayani Kyerwa wakati viongozi wakiwepo bila kuchukua hatua.
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa alisema hali hiyo inatakiwa kukoma mara moja
kutorosha madini hayo kwenda nchi jirani bila serikali kupata mapato yake.
Uzinduzin wa Miradi.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu
Mhe. Majaliwa alitembelea na kuzindua mradi wa maji Bunena ambao ujengwa katika Maispaa ya Bukoba kwa ufadhili wa
Serikali ya Ufaransa na umekamilika kwa asilimia 98% na gharama ya mradi huo ni
zaidi ya shilingi bilioni 31na unatarajiwa kukabidhiwa mwezi Aprili 2016 mara
baada ya kuwa umekamilika kwa asilimia mia moja.
Pia Waziri
Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alizindua kiwanda cha Maji cha Bunena Spring Water
ambacho kinazalisha maji ya kunywa na kimejengwa na Kanisa Katoliki
likishirikiana na wawekezaji wawili wazawa. Kiwanda hicho kina uwezo wa
kuzalisha maji safi na salaama ya kunywa chupa za Mililita 600 milioni tatu kwa
siku.
Mkutano na Watumishi wa Serikali.
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa pia aliongea na watumishi wa
Serikali Mkoani Kagera kwa kuwa kumbusha maadili ya kazi zao kwa kusema kuwa
wajibu wa mtumishi wa Serikali ni kumpokea mwananchi, kumsikiliza, na
kumhudumia au kumwelekeza mahali pa kupata huduma stahili bila kinyongo au
kukasirika.
“Najua kuwa
watumishi wa kada mbalimbali mnaidai Serikali stahiki zenu, Serikali ya awamu
ya tano imejipanga kuhakikisha inalipa madeni ya watumishi na kwasababu hiyo
nawaombeni watumishi msitumie kigezo
hicho cha kuidai serikali kufanya fujo au kukataa kuwahudumia wananchi.
Alisistiza Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa.
Mkutano wa Hadhara.
Akiongea na wananchi wa Manispaa ya
Bukoba katika uwanja wa Uhuru pamoja na kero mbalimbali walizoziwasilisha kwake
ikiwa mojawapo ni kero ya wananchi waliopimiwa viwanja 800 na hawakugawiwa
viwanja hivyo, Mhe. Majaliwa alitoa muda wa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi na
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba kuwa wawe
wametafuta utatuzi wa mgogoro huo pia aliagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa fedha za serikali kuja kufanya ukaguzi
kuhusu viwanja hivyo.
|
No comments:
Post a Comment