UNDP /TANZANIA:-Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu kuboresha Sera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, March 14, 2016

UNDP /TANZANIA:-Ripoti ya Maendeleo ya Binadamu kuboresha Sera.

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Shirika la Kazi  Ofisi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi, Bi. Mary Kawar, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez, Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Awa Dabo kwa pamoja wakiwa wameshikilia ripoti hiyo.

Muonekano wa Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015). Kwa picha zaidi bofya link hii.
Mgeni rasmi Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Mh. Anthony Mavunde (katikati) akizindua rasmi Ripoti ya Maendeleo ya Watu ya mwaka 2015 (Human Development Report 2015) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Machi 11, 2016.

SERIKALI YA TANZANIA, imesema itatumia ripoti ya Maendeleo ya Binadamu ya mwaka 2015 kama rasilimali muhimu katika kuboresha sera, mikakati na hatua mbalimbali kuhusu masuala ya kazi ikiwa ni katika kuleta maendeleo.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira na Vijana, Dk Anthony Mavunde wakati akizindua ripoti hiyo jijini Dar es Salaam. 

Alisema ripoti imehusisha kazi moja kwa moja na maendeleo ya binadamu.

Alisema ripoti hiyo yenye kauli mbiu ya ‘Kazi kwa Maendeleo ya Binadamu’ inaonesha ni jinsi gani maisha ya Mtanzania yanaweza kubadilika kupitia kazi na kumletea maendeleo. 

Hata hivyo, alisema bado kuna changamoto katika maeneo mengi ya kazi na hasa sheria zinazohusu kazi kwani wapo baadhi ya waajiri wamekuwa hawafuati sheria hizo.

Nawaagiza waajiri nchi nzima kuhakikisha wanafuata na kusimamia sheria za kazi, kwa sababu migogoro mingi katika maeneo ya kazi husababishwa na mambo mbalimbali ikiwemo kutofuata sheria,” alisema Mavunde.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad