Waziri Mkuu wa Tanzania,Bw.
Kassim Majaliwa akipokea Tuzo kutoka kwa Msanii wa filamu Elizabeth Michael
ambayo msanii huyo alishinda nchini Nigearia. Tukio hilo lilifanyika Ofisini
kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 11, 2016.
|
Waziri Mkuu wa Tanzania,Bw
Kasim Majaliwa akipokea tuzo kutoka kwa msanii wa filamu, Single Mtambalike
ambayo msanii huyo alishinda nchini Nigeria. Tukio hilo lilifanyika Ofisini kwa
Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Machi 11, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Waziri Mkuu
wa Tanzania,Bw Majaliwa, amesema hayo leo,March 11,2016 katika ukumbi wa mikutano ulipo katika Ofisi yake
Jijini Dares Salaam, alipokutana na washindi wa tuzo za filamu Afrika za mwaka 2016 (AMVCA) ambao ni
Elizabeth Michael ‘Lulu’ aliyeshinda tuzo ya Filamu Bora ya Afrika
Mashariki na Single Mtambalike ‘Richie’
aliyeshinda tuzo ya Filamu Bora ya Kiswahili pamoja Naibu Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Mhe. Annastazia Wambura,Katibu Mkuu wa
wizara Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania Bi Joyce Fisso na wasanii wa filamu.
“Serikali imefarijika sana kwa nyie kwenda
Nigeria na kushinda na mmetumia lugha ya Kiswahili, lazima tutumie nafasi hii
kuwatangaza pia mmuendelee na fani hii ili kuvutia wengi
zaidi” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
Aidha,
Waziri Mkuu amewapongeza wasanii hao na kusema kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wasanii wakati wowote na amewataka
kujipanga vizuri kutumia vyama vyao vya sanaa na kusisitiza kuwa Mhe.
Rais John Pombe Magufuli ametoa matamko kadhaa kuhusu sanaa
na wasanii na ameendelea
kushughulikia malalamiko yao ikiwemo suala la COSOTA, na kusema kuwa baada ya taratibu zote kukamilika suala hilo litasimamiwa na Wizara inayohusika
na kazi za Sanaa.
Waziri Mkuu
Majaliwa, pia amewataka watanzania kuacha tabia ya kutojiamini na kujidharau, na kuwataka watu waige mfano
kwa wasanii hao, na kuwashauri wasanii wote kwa ujumla kutumia vyombo vya
habari kujiimarisha na kujitangaza.
Kwa upande wao, wasanii waliopata tuzo hizo kwa filamu ya “Mapenzi ya Mungu”
ya Elizabeth Michael na filamu ya
“Kitendawili” ya Single Mtambalike,
wameishukuru Serikali kwa kuwathamini na
kuonesha ushirikiano katika kazi zao za
sanaa, na wameahidi kuendelea
kutengeneza kazi nzuri za sanaa
ili ziweze kuitangaza Tanzania kimataifa.
Naye, Rais
wa Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) Saimon Mwakifamba ameishukuru Serikali
kwa jitihada mbalimbali inazofanya
katika kusaidia tasnia ya sanaa kwa ujumla na ameahidi kuendelea kushirikiana
na Serikali katika kuendeleza tasnia
hiyo kimataifa.
|
No comments:
Post a Comment