Mwenyekiti
wa Chadema-Taifa Freeman Mbowe amesema,
Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea wa chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka
jana na kuungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hakutoa hata
senti moja alipojiunga na chama hicho.
Mbowe
amezungumza hayo leo March 12,2016, kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Chadema linaloendelea
hivi sasa Jijini Mwanza.
Amesema
kuwa, pamoja na kuwepo kwa kauli nyingi kwamba, Lowassa alimwaga pesa kabla ya
kujiunga na chama hicho, ukweli unabaki kuwa hakutoa pesa yoyote kama
ilivyokuwa ikidaiwa.
“Watoto
wangu walikuwa wanakula sana maharage, sasa siku moja wakala nyama, jirani
akasema umeona Lowassa kaja Chadema,” amesema Mbowe.
Akizungumzia
migogoro ya kichama iliyokuwa imejitokeza kwenye uchaguzi uliopita Oktoba 25 mwaka
huu Mbowe amesema, kuna kila sababu kushughulikia migogoro hiyo kwa haraka.
“Migogoro
mingi ndani ya Chadema imepelekea kuanguka kwa chama, hivyo itashugulikiwa kwa
haraka,” amesema na kuongeza; “Uchaguzi mkuu wa chama ni Oktoba 2018.”
Amewaeleza
wajumbe wa mkutano huo kwamba, harakati za kisiasa hasa kukikuza chama ni
gharama kubwa, jambo ambalo chama kinajitahidi kukabiliana nalo.
Amesema
kwamba, pamoja na mambo yote ndani ya chama hicho lakini suala la rushwa
haliwezi kuvumiliwa hata mara moja.
Akifafanua
kauli hiyo amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeishi kwa kulea rushwa na
kwamba, hali hiyo ndio imekifikisha hapo kilipo sasa.
Amesema,
hali hiyo inaelekea kuingia Chadema jambo ambalo linaweza kusababisha kupasuka
kwa chama hicho endapo halitashughulikiwa.
“Jambo
ambalo hatutalivumilia ndani ya Chadema ni swala la rushwa kwani rushwa inagawa
taifa, sasa swala la rushwa lililelewa na CCM na sasa inataka kuingia Chadema,”
amesema.
“Kuna
majimbo kama Iringa, Rukwa, Arusha Chadema waliachiwa kwa asilimia mia moja na
Ukawa lakini kwanini wameshindwa kuchukua ushindi wa kutosha katika majimbo
hayo?” amehoji.
Akizungumzia
changamoto za Ukawa, Mbowe amekiri kuwepo na kwamba hakuna sababu ya kuzikwepa.
|
No comments:
Post a Comment