Akizungumza
jana baada ya kumtembeza Rais huyo kwenye Eneo Maalumu la Uwekezaji la
Benjamini Mkapa (EPZ) lililopo Ubungo jijini hapa, Waziri Mwijage alisema Dk
Magufuli ametoa kibali hicho baada ya kuridhishwa na mabadiliko ya muda mfupi
ya Vietnam.
“Kutokana na
hatua waliyopiga, Rais ameniruhusu mimi na Waziri wa Kilimo, Mwigulu Nchemba
kwenda nchini humo muda mfupi baada ya Rais Truong kuondoka.
"Nitakwenda
kujifunza mbinu zao ili sekta ya viwanda iajiri zaidi ya asilimia 46 ya vijana
wa Kitanzania,” alisema Mwijage.
Baada ya
kuondolewa vikwazo na Marekani, Vietnam ilichagua kuendeleza maeneo maalumu ya
biashara na kufanikiwa kujijenga kiuchumi na kufikia uchumi wa kati katika
kipindi cha miaka 23.
Rais Truong
alieleza kuwa waliwekeza Sh10 bilioni katika miradi na asilimia 80 ya fedha
hizo ilielekezwa katika mauzo ya nje.
“EPZ zina
mchango mkubwa kwenye uchumi wetu. Ninaamini, Tanzania inaweza kupata zaidi ya
Dola 20 bilioni kwa mwaka itazipata kutoka katika maeneo haya.
"Hata
sisi wakati tunaanza tulikuwa na EPZ chache lakini sasa tunazo nyingi na
zinatuingizia dola 20 bilioni (za Marekani) kwa mwaka,”alisema.
Pamoja na
eneo hilo, Mwijage alisema Serikali ina mpango wa kuijenga Bagamoyo na kuifanya
kuwa mji wa uwekezaji.
“Taratibu za
kuwalipa wananchi ili kupisha eneo la kilomita 100 za mraba zimekamilika na
ndani ya mwaka huu mchakato huo utahitimishwa kabla wawekezaji hawajaanza
kukaribishwa,” alisema.
Kwa upande
wake, Mkurugenzi Mkuu wa EPZ, Kanali mstaafu Joseph Simbakalia alisema Serikali
imeuagiza kila mkoa kutenga eneo la uwekezaji ili kuongeza idadi ya viwanda
vilivyopo nchini.
“Kwa sasa
EPZ zinaingiza kiasi cha dola bilioni moja za Marekani (zaidi ya Sh2 trilioni)
kwa mwaka.Serikali kwa kushirikiana na Singapore imetenga dola 10 bilioni
(zaidi ya Sh20 trilioni) ambazo zitatumika kujenga mji wa Bagamoyo,” alisema
Kanali Simbakalia.
Mikoa
mingine iliyotengwa kwa ajili ya kujenga EPZ ni Kigoma, Morogoro na Mtwara.
|
Waziri wa
Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage akimtambulishaMkurugenzi Mkuu wa
EPZA, Mhe. Kanali Mstaafu Joseph Simbakalia.
|
Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Mwijage akimwelezea Rais wa Vietnam, Mhe.
Truong shughuli zinazofanywa na Kampuni ya Simu ya Halotel kutoka nchini
Vietnam, ambapo alimwonyesha Vocha za muda wa maongezi za mtandao huo ambazo
zinapatikana katika gharama tofauti kulingana na nafasi ya kifedha ya mtumiaji.
Mhe. Mwijage
akiwasilisha taarifa ya Wizara juu ya fursa za uwekezaji zilizopo nchini
Tanzania, hali halisi ya uwekezaji katika kituo cha EPZA na jitihada
zinazofanywa na Serikali katika kuanzisha maeneo ya uwekezaji katika mikoa yote
nchini kufuatia shughuli za kiuchumi zinazofaa katika Mkoa husika.
|
No comments:
Post a Comment