KLABU BINGWA ULAYA 2015/2016:- PSG, Benfica , Real Madrid na VfL Wolfsburg hizo Robo Fainali …Bado timu 4’’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, March 10, 2016

KLABU BINGWA ULAYA 2015/2016:- PSG, Benfica , Real Madrid na VfL Wolfsburg hizo Robo Fainali …Bado timu 4’’

Mshambuliaji wa PSG ya Ufaransa, Zlatan Ibrahimovic akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kuifungia timu yake bao la ushindi ,ikiilaza Chelsea 2-1 usiku wa Jumatano March 09, 2016,kwenye Uwanja wa Stamford Bridge na kutinga Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa jumla wa 4 -2.
Mchezo wa awali PSG ilishinda pia 2-1 mjini Paris. Bao lingine la PSG limefungwa na Adrien Rabiot, wakati la Chelsea limefungwa na Diego Coasta.

Chelsea ambayo ipo katika nafasi ya 10 katika jedwali la ligi ya Uingereza sasa inakabiliwa na tishio la kutoshiriki katika ligi ya bara Ulaya msimu ujao,huku Costa na Eden Hazard wakitolewa katika mechi hiyo na jeraha kabla ya mechi ya robo fainali ya FA dhidi ya Everton.

Huko Urusi,Wenyeji Zenit St Petersburg walichapwa 2-1 na Benfica na kutupwa nje.
 

Paris St Germain na Benfica zinaungana na Real Madrid na VfL Wolfsburg kutinga Robo Fainali.


Mechi za Marudiano za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za Ligi hiyo zitakamilika Wiki ijayo kwa Mechi 4 za mwisho.


TIMU ZILIZOFUZU KUINGIA ROBO FAINALI



-Real Madrid

-VfL Wolfsburg

-Paris St Germain

-Benfica

**Bado Timu 4





RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16



**Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza



JUMANNE 15 MAR 2016



Atletico Madrid v PSV Eindhoven [0-0]



Man City v Dynamo Kiev [3-1]   



JUMATANO 16 MAR 2016



Barcelona v Arsenal [2-0]



Bayern Munich v Juventus [2-2]



++++++++++++++++++++++++++++



TAREHE MUHIMU



Raundi za Mtoano:



-Droo ya Robo Fainali: Machi 18



**Mechi Aprili 5/6 na Marudiano Aprili 12/13



-Droo ya Nusu Fainali: Aprili 15



**Mechi Aprili 26/27 na Marudiano Mei 3/4



FAINALI



Mei 28,2016.



San Siro, Milan, Italy

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad