Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na ungozi wa juu wa Benki Kuu ya
Tanzania ambao ameupa maelekezo mbalimbali katika kuboresha utendaji wao wa kazi wakila siku.
|
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akikagua CV za wafanyakazi wa Benki Kuu ya
Tanzania wakati wa ziara yake ya
kushtukiza jijini Dar es Salaam. Kulia kwake ni Gavana wa Benki Kuu Beno Ndulu.
|
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya ziara ya
kushitukiza katika Benki Kuu ya Tanzania (BOT), ambapo pamoja na mambo mengine
ameiagiza Benki hiyo kusitisha mara moja ulipaji wa malimbikizo ya malipo
ambayo tayari yalishaidhinishwa (Ex-Checker) na badala yake yarejeshwe Wizara
ya fedha na Mipango kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.
Mpaka Rais
Magufuli anatoa agizo hilo, Benki Kuu ya Tanzania ilikuwa katika mchakato wa
kufanya malipo ya shilingi Bilioni 925.6, ambazo Wizara ya Fedha ilitoa idhini
ya kufanyika malipo.
Akizungumza
na watendaji wakuu wa Benki Kuu ya Tanzania waliojumuisha Gavana, Naibu Magavana,
Wakurugenzi na Mameneja, Rais Magufuli ametaka Wizara ya Fedha ifanye upya
uhakiki wa malipo hayo, ili kubaini kama walengwa walioidhinishwa kulipwa
wanastahili kulipwa ama vinginevyo.
Aidha, Dkt.
Magufuli ameagiza Kitengo cha madeni ya nje ambacho awali kilikuwa chini ya
Benki Kuu na baadaye kikahamishiwa Wizara ya Fedha, kirejeshwe Benki Kuu mara
moja ili kuimarisha udhibiti wa ukopaji na ulipaji wa madeni.
Wakati huo
huo, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania
Prof. Beno Ndulu kupitia upya orodha ya wafanyakazi wa Benki hiyo, na kuwaondoa
mara moja wale wote ambao hawana ulazima wa kuwa wafanyakazi katika benki hiyo.
"Haiwezekani
tukawa na kundi kubwa la wafanyakazi, wanalipwa mishahara wakati hata kazi
wanazofanya hazijulikani" Amesema Dkt. Magufuli.
Rais
Magufuli ametoa agizo hilo wakati ambapo Benki Kuu ya Tanzania ina wafanyakazi
1391.
Gerson
Msigwa
Kaimu
Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es
salaam-10 Machi, 2016.
|
No comments:
Post a Comment