Kiiza (Pichani ) amefikisha mabao 18 baada
ya kufunga bao mbili kwenye mchezo kati ya Simba dhidi ya Ndanda FC. Kiiza
anamzidi Amis Tambwe wa Yanga mwenye mabao 17 aliyofikisha baada ya kufunga
magoli mawili wakati Yanga SC iliposhinda kwa magoli 5-0 dhidi African Sports.
‘Wekundu wa
Msimbazi’ Simba SC wameendelea kufanya Vyema kwenye Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Msimu
huu 2015/2016,kufuatia ushindi mnono wa magoli 3 - 0 dhidi ya Ndanda FC ya
Mtwara kwenye mchezo wao wa marudiano uliochezwa kwenye uwanja wa taifa,Jijini
Dar es Salaam leo March 10, 2016,Jioni.
Simba SC ilianza kupata bao la kwanza lililofungwa na
Mwinyi Kazimoto dakika ya 32 akiunganisha vizuri krosi ya Ibrahim Ajib huku Dakika
ya 52 Kiiza angafunga bao la pili ambalo lilikuwa ni bao lake la 17 kwenye Ligi,
Kiiza aliunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa na Ibrahim Ajib.
Kiiza aliifungia
Simba SC bao la tatu na kuchukua usukani wa wafungaji bora wa VPL baada ya
kuunganisha pasi ya Danny Lyanga aliyeuwahi mpira uliotemwa na golikipa wa
Ndanda kufuatia shuti kali la mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Justice
Majabvi.
SimbaSC imefikisha jumla ya pointi 51 baada ya kucheza michezo 22 na kurudi
kileleni mwa ligi kwa mara nyingine wakiitoa Yanga SC yenye pointi 50 ikiwa
imecheza michezo 21.
|
Mchezo mwingine wa Ligi Kuu leo,March 10,2016 Mbeya City Imeifunga 2-0 Stand United
Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, mabao ya Raphael Daudi na Haruna Shamte.
Matokeo yote ya mechi za VPL zilizochezwa March 09, 2016, yapo kama ifuatavyo.
Mwadui FC 0 -
0 Majimaji FC
Tanzania
Prisons 1 - 1 Kagera Sugar
Coastal
Union 1 - 0 Mgambo JKT
JKT Ruvu 2 -
0 Toto Africans
|
No comments:
Post a Comment