Serikali
imetakiwa kuboresha mazingira bora ya walimu ili kukuza na kuboresha kiwango cha
elimu nchini kwani walimu ni kiungo muhimu katika elimu ambacho kinapaswa
kupewa kipaumbele kwenye kutimiza azma ya serikali kutoa elimu bora kwa Watanzania.
Mkurugenzi
wa Shirika lisilokua la kiserikali la
The Foundation for Tomorrow (TFFT)
,Melissa Queyquen ameyasema hayo jana,February 09,2016 wakati wa utoaji wa tuzo
za walimu bora wa shule za msingi za serikali kwa kutambua mchango wa walimu
katika maendeleo ya elimu nchini na ustawi bora wa jamii .
Melisaalisema
kuwa maendeleo ya taifa lolote lile yanategemea ubora wa elimu waliyonayo watu
wake hivyo ni vyema serikali inapofikiria kuboresha elimu ifikirie kuboresha
mazingira ya walimu kuanzia kitaaluma wanapoandaliwa kwenda kufundisha ,vifaa
vya kufindishia pamoja na stahiki zao.
“Bila Walimu
Bora hakuna Elimu Bora ,Tumeamua kuwatia moyo wa walimu kwa kutoa tuzo hizi na
vyeti vya kutambua mchango wao, washindi ni 10 mshindi wa kwanza amepatiwa
cheti na shilingi la kitano,na washindi wengine tumewapatia vyeti na fedha
taslimu” Alisema Melisa.
Afisa Elimu
wa Shule za Msingi Wilaya ya Meru Tumsifu Mushi
amewataka walimu kufanya kazi ya ualimu kwa moyo na kwa kujituma huku
wakitambua kuwa wana wajibu mkubwa wa kuandaa wataalamu watakaoisaidia
jamii,taifa na duni jukumu ambalo ni nyeti linapaswa kubebwa kwa uzito
unaostahili.
Kwa upande
wao walimu waliopewa tuzo hizo Rose Salim wa shule ya Msingi Uraki na Ekaeli
Newasha wa Shule ya msingi Kimundo wamesema kuwa kundi la walimu limekua
likisahaulika mchango wake katika jamii hivyo tuzo hizo Zimeamsha ari na hamasa ya kufanya kazi kwa bidii.
“Kazi ya
ualimu unapaswa uwe unapenda watoto
unapenda kuwasaidia waweze kufika mbali kitaaluma ,binafsi nimefanya
kazi hii kwa miaka mingi na ninaipenda sana” Alisema Mwalimu Rose Salim.
Imeandaliwa
na Ferdinand Shayo wa Wazalendo 25 Blog ,Arusha.
|
Afisa Elimu
wa Shule za Msingi wilaya ya Arumeru Tumsifu Mushi akizungumza katika utoaji wa
tuzo za Walimu Bora na jumla ya walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10
walipatia tuzo nazawadi mbalimbali.Picha na Ferdinand Shayo.
|
Washindi wa
tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika
lisilokua la kiserikali la The
Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa
Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya
walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
|
Washindi wa
tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika
lisilokua la kiserikali la The
Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa
Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya
walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
|
Mkurugenzi
wa Shirika lisilokua la kiserikali la
The Foundation for Tommorrow (TFFT)
,Melissa Queyquen akizungumza na walimu katika Halfa ya Utoaji tuzo za walimu
bora kwa walimu wa shule za msingi wilaya ya Meru zilizofanyika jana ,february 09,2016 ,jumla ya
walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
|
Washindi wa
tuzo za walimu bora wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika
lisilokua la kiserikali la The
Foundation for Tommorrow (TFFT) ,Melissa
Queyquen akishuhudia tukio hilo lililoandaliwa na shirika lake .,jumla ya
walimu 200 wameshiriki ambapo walimu 10 walipatia tuzo na zawadi mbalimbali.
|
No comments:
Post a Comment