Tume ya
Taifa ya Uchaguzi nchini NEC imebainisha kwamba, ukosefu wa elimu ya kutosha
kwa Wapiga Kura, ulisababisha mapungufu mbalimbali kujitokeza katika uchaguzi
Mkuu uliofanyika Octoba 25 Mwaka jana,2015.
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Kailima Ramadhani (Pichani juu) aliyasema hayo jana,February 09,2016,
Jijini Mwanza, katika Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu
utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana,2015.
Ramadhani
alisema katika baadhi ya Kata nchini, kulitokea mapungufu kadhaa katika zoezi
la kupiga kura ikiwemo Kura kuharibika kutokana na wapiga kura kuchora michoro
na alaza zisizostahili katika karatasi ya kupigia kura huku baadhi yao
wakiandika matusi katika karatasi hizo.
Hata hivyo
Kailima alitanabaisha kwamba, zoezi la utoaji wa elimu kwa mpiga kura,
lilishindwa kufanikiwa zaidi kutokana na baadhi ya Asasi za kiraia nchini kutoa
elimu kinyume na mwongozi wa NEC, ambapo baadhi ya Asasi hizo zilikuwa zikitoa
elimu ya mpiga kura kwa kuangazia zaidi matakwa ya wafadhiri wake.
Edwin Soko
ambae ni mmoja wa Wadau kutoka Asasi zilizohudhuria katika Mkutano huo ambao
umejumuisha Asasi mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa, amesema kuwa katika
Uchaguzi wa Mwaka jana 2015, Asasi nyingi hazikuweza kuyafikia maeneo mengi hususani
vijijini kwa ajili ya Kutoa elimu ya Mpiga kura, hii ikiwa ni kutokana na
ukosefu wa fedha ambapo wameishauri Serikali kuwa na utaratibu wa kutoa ruzuku
kwa asasi hizo ili kutoa elimu hiyo katika chaguzi zijazo.
Kando ya
Tathmini hiyo, Suala la Kuahirishwa kwa Uchaguzi Visiwani Zanzibar
likajitokeza, ambapo Wanahabari walitaka kujua sababu za Uchaguzi huo
kuahirishwa, na hapo ndipo Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka NEC akatumia tena
fursa hiyo kufafanua kwamba Uchaguzi Visiwani Zanzibar uliahirishwa na Tume ya
Uchaguzi Visiwani humo ZEC kutokana na tume hiyo kubaini kasoro kadhaa katika
karatasi zake za wapiga kura, kasoro ambazo hata hivyo hazikujitokeza katika
karatasi zilizokuwa zikisimamiwa na Tume ya Uchaguzi nchini NEC ikizingatiwa
kwamba ZEC na NEC ni tume mbili tofauti zisizoingiliana katika majukumu.
|
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akizungumza na Wanahabari Jijini
Mwanza nje ya Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji
wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana 2015.
|
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume hiyo Kailima Ramadhani akizungumza na Wanahabari Jijini
Mwanza nje ya Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji
wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana,2015.
|
Wadau
mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC
na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu
wa Mwaka jana,2015.
|
Wadau
mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini kati ya NEC
na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu
wa Mwaka jana,2015.
|
Wanahabari
na Wadau mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa Mkutano wa tathmini
kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya Mpiga Kura wakati wa
Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana,2015.
|
Wadau
mbalimbali kutoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa katika picha ya pamoja wakati
wa Mkutano wa tathmini kati ya NEC na Asasi za Kiraia kuhusu utoaji wa elimu ya
Mpiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Mwaka jana,2015.
|
Kutoka
Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju
(Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC),
Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi
NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Geita.
|
Kutoka
Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju
(Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC),
Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi
NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Kagera.
|
Kutoka
Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju
(Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC),
Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi
NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Mwanza.
|
Kutoka
Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju
(Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC),
Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi
NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Shinyanga.
|
Kutoka
Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju
(Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC),
Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi
NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Mara.
|
Kutoka
Kushoto Waliokaa ni Abel John (Afisa Elimu ya Mpiga Kura NEC), Maryam Ukwaju
(Afisa Uchaguzi Jijini Mwanza), Kailima Ramadhani (Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC),
Moses Pesha (Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Mwanza) na Mary Mchome (Afisa Ugavi
NEC) Wakiwa pamoja na Wadau kutoka Mkoani Simiyu.
|
Imeandaliwa
na George Binagi-GB Pazzo wa Binagi Media Group.
|
No comments:
Post a Comment