EMIRATES FA CUP 2015/2016:- Liverpool yatolewa na West Ham. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, February 10, 2016

EMIRATES FA CUP 2015/2016:- Liverpool yatolewa na West Ham.


West Ham Hapo Jana,February 09,2016 huko Upton Park iliitoa Liverpool 2-1 katika Raundi ya 4 ya EMIRATES FA CUP baada ya Kichwa cha Dakika ya 121 cha Angelo Ogbonna kuwapa ushindi.


West Ham waliongoza Bao 1-0 hadi Haftaimu kwa Bao la Dakika ya 45 la Michail Antonio alipounganisha Krosi ya Enner Valencia na Liverpool kusawazisha Dakika ya 48 kwa Frikiki ya Philippe Coutinho.

Hadi Dakika 90 kumalizika Bao zilibaki 1-1 na ndipo zikaongezwa Dakika za Nyongeza 30 na West Ham kufunga Bao lao la ushindi mwishoni.


West Ham wamesonga Raundi ya 5 na watacheza Ugenini hapo Februari 21 na Blackburn Rovers.

EMIRATES FA CUP RATIBA.

Raundi ya 4 Marudiano

Jumatano Februari 10,2016.

2245 Peterborough v West Brom

Raundi ya 5

Jumamosi Februari 20,2016.

1545 Arsenal v Hull           

1800 Reading v West Brom au Peterborough  

1800 Watford v Leeds       

2015 Bournemouth v Everton      

Jumapili Februari 21

1700 Blackburn v West Ham        

1800 Tottenham v Crystal Palace

1900 Chelsea v Man City             

Jumatatu Februari 22,2016.

Shrewsbury v Man United

THE EMIRATES FA CUP 2015/2016

TAREHE MUHIMU

Raundi ya 3

Ijumaa 9 Januari 2016

Raundi ya 4

Jumamosi 30 Januari 2016

Raundi ya 5

Jumamosi 20 Februari 2016

Raundi ya 6-Robo Fainali

Jumamosi 12 Machi 2016

Nusu Fainali

Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016

Fainali

Jumamosi 21 Mei 2016.
Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630 Or +255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad