TASWIRA PICHA:-DR Congo mabingwa wa CHAN -2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 08, 2016

TASWIRA PICHA:-DR Congo mabingwa wa CHAN -2016.

Na huu ni ubingwa wa pili kwa timu ya taifa ya Dr Congo chini ya mwalimu Florent Ibenge kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.

DRC wamerudia mafanikio ya mwaka 2009 walipotwaa ubingwa wa fainali za kwanza za CHAN nchini Ivory Coast.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ndiyo mabingwa wa Michuano ya Ubingwa wa Mataifa (CHAN 2016), inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee baada ya kuifunga Mali mabao 3-0 katika fainali ya michuano ya mwaka huu Uwanja wa Amahoro, Kigali, nchini Rwanda,Jana February 07,2016.

Na kwa ushindi huo, Kongo wamepatiwa dola za Kimarekani 750,000 wakati Mali wamepata dola 400,000 kwa kumaliza nafasi ya pili. 

Ivory Coast waliomaliza nafasi ya tatu na Guinea wa nne, kila timu imepata dola 250,000.
Kocha wa DRC, Frolent Ibenge .

Elia Meschack alifunga dakika ya 28 na 62 kabla ya Jonathan Bolingi kufunga la tatu dakika ya 73 kuifanya DRC itwae taji la pili katika fainali za nne tangu kuanzishwa kwa CHAN.

Ikumbukwe DRC ndiyo mabingwa wa fainali za kwanza za CHAN mwaka 2009 nchini Ivory Coast.
Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, Ivory Coast iliifunga mabao 2-1 Guinea na kunyakua Medali ya Shaba.

Mabao ya Ivory Coast yamefungwa na Mohamed Youla aliyejifunga dakika ya 33 na Gbagnon Anice Badie dakika ya 35, wakati la Guinea lilifungwa na Aboubacar Leo Camara dakika ya 86.

Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630 Or+255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad