MAAFA/PICHA:-Zaidi ya Kaya 60 Wilayani Lindi Zaathiriwa na Mvua. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 08, 2016

MAAFA/PICHA:-Zaidi ya Kaya 60 Wilayani Lindi Zaathiriwa na Mvua.

Zaidi ya Kaya 60 za Vitongoji vya Kiwalawala na Mjimwema Kata ya Kitomanga Wilayani Lindi Zimeathiriwa na Mvua Zilizoambatana na Mafuriko Huku watu 94 wakifanikiwa Kuokolewa Kufuatia Jitihada za Halmashauri ya wilaya Ya Lindi kupeleka Boti kusaidia zoezi la Uokoaji.

Mvua hizo zilizonyesha Mwanzoni mwa wiki hii Tayari Maeneo mbalimbali ya wilaya Hiyo pamoja na Wilaya ya Kilwa kukosa sehemu za Kuishi huku jitihada za Kuokoa waliozungukwa na Maji zikiendelea.

Mwandishi wwetu ilifika katika Maeneo Jirani na kijiji Cha Mjimwema jirani na Kitongoji wanachoishi wafugaji na Kushuhudia zoezi la Uokoaji Likiendelea .

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi, Bi Oliva Vavunge akiongea wakati wa zoezi hilo la Uokoaji likiendelea, amewataka wananchi wote wanaoishi sehemu za mabondeni kuhama mara moja kwani Mvua hizo bado zinaendelea kunyesha kama ilivyotangazwa na mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA.

Sambamba na Tukio Hilo Mkurugenzi Mtendaji pia amewataka wakazi wanaoishi katika Bonde la Mto Lukuledi Kuanza Kuondoka katika Bonde Hilo Ili kunusuru Maisha yao pamoja na Mali zao.
Diwani wa kata Ya Kitoanga alitoa ombi kwa Kitengo cha Maafa kutoa msaada wa haraka kwa wahanga hao.

Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630 Or+255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad