WATENDAJI
wakuu wa mashirika mawili makubwa ya Umoja wa Mataifa ya Shirika la Umoja wa
Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA) na Shirika la Kimataifa
la Kuhudumia watoto (UNICEF) wametoa wito kwa dunia kujipanga vyema kumaliza
kabisa tatizo la ukeketaji (FGM) ifikapo
mwaka 2030.
Katika kauli
zao walizotoa katika taarifa ya pamoja
iliyotolewa na ofisi ya Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa mjini
Dar es salaam watendaji hao Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dk.
BabatundeOsotimehin, na Mkurugenzi
Mtendaji wa UNCEF, Anthony Lake, wamesema ipo haja ya dunia kuadhimisha siku
hiyo kwa kulenga kuwa na kiwango sifuri katika vitendo vya ukeketaji.
Mashirika
hayo ya Umoja wa Mataifa yamesema kwamba
ukeketaji ni vitendo vya kikatili vinavyowanyima wanawake haki yao ya msingi na
kuwazuia kuchanua inavyostahili kama wanawake.
Viongozi hao
wamesema kwamba vitendo vya ukeketaji vimesambaa duniani kote kuanzia Afrika,
Mashariki ya Kati ambako imekuwa kama vitu vya kawaida vikiathiri pia familia
katika nchi za Asia Australia, Ulaya, Amerika ya Kaskazini na Kusini.
Wamesema
kwamba kama hatua zisipochukuliwa kutokomeza ukeketaji idadi ya mabinti na
wanawake wanaoweza kuingizwa katika mkumbo huo itakuwa inaongezeka ikiwapeleka
katika mzunguko ule ule wa kushamirisha ukeketaji na kurejesha nyuma maendeleo
ya wanawake na binadamu kwa ujumla kama familia.
“ Ili kuhami utu wa mwanamke, tunahitaji
kuchukua hatua sasa na kuwajibika kama dunia kutokomeza ukeketaji. “ ilisema
sehemu ya taarifa ya viongozi hao kwa vyombo vya habari.
Septemba
mwaka jana katika mkutano wa kutengeneza mpango wa kimataifa wa maendeleo
endelevu, nchi 193 zilikubaliana kuhakikisha kwamba ukeketaji unakuw aumetokomezwa
ifikapo mwaka 2030.
Taarifa hiyo
imesema kwamba ili kufanikiwa wananchi wanatakiwa kushawishi familia nyingi
duniani hapa kuachana na tabia ya ukeketaji.
“Tunahitaji kufanyakazi na idadi kubwa ya wataalamu wa tiba katika jamii
zetu – wakiwemo waganga wa jadi na wataalamu wa kisasa wa matibabu,
tukiwashawishi wakatae kutoa huduma ya ukeketaji.” Ilisema taarifa hiyo.
Aidha
taarifa hiyo hiyo imetaka wanawake waliofanyiwa ukeketaji kusaidiwa huduma
mbalimbali zikiwamo za kisaikolojia na nyingine zinazostahili ili kuwapunguzia
maumivu waliyoyapata na wanayoendelea kuyapata kutokana na kukeketwa.
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 Or+255756830214.
|
No comments:
Post a Comment