LIGI KUU VODACOM 2015/2016:-Msimamo wa Ligi ufahamu wakati Mbeya City yaifumua 2-1 JKT Ruvu leo February 04,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 04, 2016

LIGI KUU VODACOM 2015/2016:-Msimamo wa Ligi ufahamu wakati Mbeya City yaifumua 2-1 JKT Ruvu leo February 04,2016.


Timu ya Mbeya City imezinduka baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya JKT Ruvu mchana wa leo February 04,2016 kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2015/2016.


Ushindi huo, unaifanya timu hiyo ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya kufikisha pointi 17 baada ya kucheza mechi 17 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya 10, wakiishusha Kagera Sugar yenye pointi 15 za mechi 17 pia.

Katika mchezo huo wa leo, Mbeya City walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 23 kupitia kwa Hassan Mwasapili na Yohanna Morris dakika ya 45 huku JKT Ruvu ilipata bao lao dakika ya 38 kupitia kwa Mussa Juma aliyefumua shuti kali baada ya kupata pasi ya kiungo wa zamani wa Yanga SC, Hassan Dilunga.

Hapo jana February 03,2016, Mabingwa watetezi Yanga SC walitoka  Sare ya bao 2-2 wakiwa  huko Sokoine Jijini Mbeya na Tanzania Prisons.


Nao, Simba SC waliinyuka Mgambo JKT 2-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam na kufikisha Pointi 39, sawa na Azam FC, na Pointi 1 nyuma ya Yanga SC wenye pointi 40.



LIGI KUU VODACOM 2015/2016 RATIBA.

Jumamosi Februari 6,2016.

Kagera Sugar v Simba SC

African Sports v Stand United

Jumapili Februari 7,2016.

Mbeya City v Tanzania Prisons

JKT Ruvu v Yanga SC

Ndanda FC v Mtibwa Sugar        

Azam FC v Mwadui FC     

Toto Africans v Coastal Union     

Majimaji v Mgambo JKT


Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp -/.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad