CHAN 2016:- Mali yafuzu kwa fainali dhidi ya DRC Jumapili February 07. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 04, 2016

CHAN 2016:- Mali yafuzu kwa fainali dhidi ya DRC Jumapili February 07.

Timu ya Mali imefuzu kushiriki fainali ya michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika miongoni mwa wachezaji wanaoshiriki ligi za nyumbani CHAN-2016 dhidi ya Congo DR baada ya kuilaza Ivory Coast 1-0 katika nusu fainali ya pili iliyochezwa katika uwanja wa taifa wa Rwanda jioni ya leo February 04,2016.

Mali ambayo ilikuwa imefuzu kwa nusu fainali yake ya kwanza ya CHAN ilipata bao la ushindi zikiwa zimesalia dakika mbili tu mechi hiyo ikamilike,kupitia kwa YVES BISSOUMA kunako dakika ya 88'ya kipindi cha pili.

Timu hiyo sasa ya Mali itacheza  dhidi ya Congo DRC katika fainali siku ya jumapili, February 07,2016 .

Leopards ya Congo DR ambaye ilimtoa Guinea kwa mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti hapo jana,Jumatano February 03,2016.

Guinea kwa upande wake sasa itachuana dhidi ya Ivory Coast kuamua mshindi wa tatu.
Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630-/+255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad