Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mhe.John Pombe Joseph Magufuli ameidhinisha
kuanzishwa kwa Mkoa mpya wa Songwe na Wilaya nyingine mpya nchini.
Akitoa tamko
hilo kwa niaba ya Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa(TAMISEMI) Mhe George Simbachawene amesema kwa mujibu wa Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 imempa Mamlaka Rais ya kugawa
Nchi kwa kadri ambavyo atakapoona inafaa.
Mhe George
Simachawene amesema kutokana na mamlaka hayo aliyopewa Rais jumla ya Wilaya
sita na Mkoa mmoja wa Songwe umeanzishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Mkoa mpya wa Songwe umeanzishwa kutoka
Mkoa wa Mbeya.
Amezitaja
Wilaya mpya zilizoanzishwa kuwa ni Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe,Wilaya ya
Ubungo Mkoa wa Dar es salaam, Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani, Wilaya ya
Kigamboni Dar es salaam, Wilaya ya Mlanyi Mkoa wa Morogoro na Wilaya ya
Tanganyika Mkoa wa Katavi
“ Nichukue
fursa hii kuwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Wilaya mpya zimeanzishwa kufanya
maandalizi rasmi ili Mkoa na Wilaya hizo ziweze kuanza kufanya kazi,aidha mkazo
uwekwe kwenye upatikanaji wa Ofisi na huduma zote muhimu kupatikana kwa urahisi
katika Mkoa naWilaya hizo mpya” Alisema Mhe Simbachawene.
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp+255789925630-/+255756830214.
|
No comments:
Post a Comment