![]() |
|
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Chama cha Maadili na Uwajibikaji (CM-TANZANIA) Bwana Laban
Nkembo amesema kuwa, chama hicho kimeanzishwa kwa lengo la kuiweka Tanzania
kimaadili na uwajibikaji kwa kuwa kinabeba mambo makubwa mawili yakiwemo Amani
na Upendo.
Ameongeza
kuwa, chama chao sio cha Upinzani na kinaheshimu chama kilichopo madarakani
hivyo, kinaahidi kushirikiana na Chama Tawala kuenzi mazuri yanayofanywa na
chama hicho.
‘’Chama chetu sio cha upinzani, tunataka nchi
nyingine duniani ziwe zinakuja kujifunza Tanzania kuhusu amani na maendeleo
tulionayo’’, alisema Nkembo.
Aidha,
amebainisha kuwa, chama chao cha CM-TANZANIA kitatoa ajira za kudumu kwa
Wanachama wake na hata kwa wale wasiokuwa wanachama ambapo kimeshaandaa Idara
ya usimamizi mzuri wa huduma kwa jamii kama vile Wazee, Wajane, Walemavu pamoja
na Yatima.
CM-TANZANIA
ni Chama cha 23 kupokea usajili baada ya Vyama vingine vya siasa 22 vyenye
usajili wa kudumu.
|
Thursday, February 04, 2016
HARAKATI ZA VYAMA TANZANIA:-Fahamu Usajili kwa Chama kipya cha CM -TANZANIA..
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.







No comments:
Post a Comment