![]() |
Rais wa Tanzania, Dk.
John Magufuli amesema anapochukua hatua yeye si kichaa, si dikteta, si shetani
wala si mnyama, ila ni mpole, lakini amefika mahali lazima afanye hivyo kwani
ndani ya Serikali yanafanyika mambo ya ajabu.
Kauli hiyo
aliitoa jana jijini Dar es Salaam katika kilele cha Siku ya Sheria nchini,
alipokuwa mgeni rasmi kwa mara ya kwanza katika uzinduzi wa Mwaka wa Mahakama
tangu alipoapishwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisifu kazi
kubwa inayofanywa na Idara ya Mahakama, huku akitangaza uamuzi wa gharama za
kurusha matangazo ya moja kwa moja ya Bunge zaidi ya Sh bilioni nne ni bora
zikawasaidia wananchi.
“Ninapochukua
hatua mimi si mnyama, si dikteta, si shetani, ni mpole kweli, lakini inafika
mahali lazima nifanye, yanayofanyika serikalini ni mambo ya ajabu sana, nataka
kutoa sadaka yangu, inawezekana hata nikifa naweza kuwa rais wa malaika,”
alisema.
Alipongeza
kazi kubwa inayofanywa na mahakama huku akibaki kujiuliza kwanini katika
maadhimisho ya siku yao hawarushi matangazo yao moja kwa moja kupitia luninga.
“Mnafanya
kazi kubwa, nilipofika niliuliza kwanini hii siku yenu hamrushi ‘live’,
nikajibiwa fedha za kurusha ‘live’ zinapelekwa kuwahudumia wananchi.
“Kipindi
kimoja kurusha ‘live’ kwa wiki mbili inatumika zaidi ya Sh bilioni nne, ni
vizuri kuzikata hizo fedha zinazopelekwa kurusha ‘live’ zikapelekwa katika kesi
za ubunge zinazohitaji shilingi bilioni tatu kusikilizwa hadi kumalizika
kwake,” alisema.
Alisema
mahakama ilikuwa inapewa bajeti ya Sh bilioni 41, lakini mwaka 2015/2016
ilishuka wakatakiwa kupewa Sh bilioni 12 ambazo hadi sasa hawajapewa.
“Kiongozi
lazima ufikirie wapi pa kupeleka fedha na wapi pa kunyima, watu wa mahakama
mnafanya kazi ya Mungu, nawaahidi ndani ya siku tano nitakuwa nimewapa Sh
bilioni 12 zote.
“Sina tatizo
la masilahi ya wafanyakazi wa mahakama, katika bajeti ya mwaka huu nitawapa
fedha nyingi kuliko bajeti zote zilizopita, fedha zipo,” alisema.
Mahakimu
Kutumbuliwa.
Rais Magufuli
alisema anamwagiza Jaji Mkuu kuwachukulia hatua mahakimu 502 ambao hawakufikia
malengo ya kumaliza kesi 250-260 kwa mwaka. Walimaliza kesi chini ya 100.
“Mahakimu
ambao hawajafikia kumaliza kesi 260 hayo ndiyo majipu yako Jaji Mkuu, unatakiwa
kuyatumbua, wewe uliniapisha hata mimi, leo unapitisha agizo mwingine anapinga.
“Unatoa siku
saba sasa sijui ndiyo watamaliza kutoa hizo hukumu, nakuagiza wachukulie hatua,
tusipochukua hatua hakuna kitakachofanyika.
“Walioshindwa
kufikia lengo unawabakiza wa nini, wasomi wako wengi, hata ukitangaza leo
watajitokeza, niruhusu mimi nitangaze, sitaki kuingilia mahakama,” alisema.
Mabilioni ya
NIDA.
Akizungumzia
hatua yake kwa watendaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), alisema
ilipewa Sh bilioni 176.6, lakini vitambulisho vilivyotengenezwa havifiki hata
milioni mbili na havina sahihi wakati vitambulisho vya kupigia kura fedha
iliyotolewa haizidi Sh bilioni 70, lakini vina sahihi za wapigakura wote wa
Tanzania ambao ni milioni 23,253,982.
“Utaona ugumu
wa kuongoza, nchi inatawaliwa na madudu ya kila aina, wapo watu wanacheza na
fedha wanavyotaka wakati wapo watu masikini sana, wengine wanataka bodi zao
wakakae Ulaya.
“Hapo ndipo
tulipofikia, wengine wanalipwa mshahara kwa mwezi Sh milioni 35, naomba mniombee
kabla ya kunihukumu, toeni hukumu kwa haki kwa hawa wanaotaka kuifikisha nchi
pabaya, toeni hukumu zao haraka,” alisema.
Kesi za
Wakwepa kodi.
Rais
Magufuli alisema kuna kesi 442 za kukwepa kodi ambazo zingeamuliwa Serikali
ingepata Sh trilioni moja, ambayo ingeweza kununua ndege zaidi ya sita.
Alimuomba
Jaji Mkuu kuzimaliza kesi 442 na kama zikimalizika fedha hizo Sh trilioni moja
ataipa Idara ya Mahakama Sh bilioni 259 na Sh bilioni 750 zilizobakia
zitanunuliwa ndege sita na wafanyafakazi 250 ATCL waliopo sasa wataondolewa.
Akizungumzia
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, alisema kuna kesi 26 za watu waliokutwa na
nyara za Serikali, ambazo zipo zaidi ya miaka mitano hazijaamuliwa kwa sababu
upelelezi bado.
“Polisi
wapo, DPP yupo, upelelezi unaendelea kila siku, hapo unaona tatizo lilipo, DPP
upo unapeleleza nini au unatafuta rushwa?” alisema.
Alisema
suala la kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi ya wahujumu uchumi halihitaji
kwenda bungeni kufanya mabadiliko, lifanywe haraka, mahakama ianze kwani nchi
inachezewa.
Pamoja na
hali hiyo Rais Magufuli alikubali kupokea maombi yote yaliyotolewa na mahakama
na kuyazingatia kwani lazima ayaunge mkono ikiwamo kukubali watumishi wa Idara
ya Mahakama wasome na kupatiwa mikopo na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu
ya Juu (HESLB).
“Nimeamua
nchi iende na itaenda, anayefikiria ataikwamisha atakwama yeye, nategemea zaidi
mahakama katika kufanikisha hilo,” alisema.BOFYA HAPA KUSIKILIZA-HOTUBA YA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI, RAIS WA TANZANIA SIKU YA SHERIA 2016.
|
Friday, February 05, 2016
Home
HABARI
AUDIO/PICHA:-Rais Magufuli Asema si Kichaa wala Dikteta, Kuifanyia Mema Nchi ya Tanzania.
AUDIO/PICHA:-Rais Magufuli Asema si Kichaa wala Dikteta, Kuifanyia Mema Nchi ya Tanzania.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.







No comments:
Post a Comment