|
Waziri wa
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiteta jambo na Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa Mhe.Dkt Hussein Ali Mwinyi wakati wa katika
kikao cha 9 cha Bunge la 11 Mjini Dodoma….Picha
na Raymond Mushumbusi – MAELEZO.
Aidha, Mhe
Kassim Majaliwa,Majaliwa amesema
Serikali kwa kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) inaendelea
kujenga maghala ya kimkakati kwa ajili ya kuhifadhi akiba ya Taifa na kwa sasa
ghala moja lenye uwezo wa kuhifadhi Tani 5,000 limeshajengwa Wilayani Mbozi
Mkoani Mbeya na Serikali imepata mkopo wenye masharti nafuu kutoka Serikali ya
Poland ambao utawezesha kujenga vihenge vya kisasa (silos) vyenye uwezo wa
kuhifadhi Tani 160,000 na maghala yenye uwezo wa kuhifadhi Tani 90.
Ameongeza
kuwa Pamoja na hatua zinazochukuliwa na Serikali, amewataka viongozi wa Mikoa,
Wilaya na watendaji katika Halmashauri zote Nchini kuwahamasisha Wananchi
kutumia vizuri mvua zinazonyesha nchini kote kwa kulima kwa bidii ili kuweza
kuvuna na kujiwekea akiba ya chakula cha kutosha kwa ajili ya kaya zao wakati
wote wa mwaka na wawahamasishe wafanyabiashara na wadau wengine kusaidia
Serikali kuchukua chakula kutoka maeneo yenye ziada na kupeleka katika maeneo
yenye upungufu na kwa kuzingatia maelekezo haya pamoja na juhudi za Serikali
zilizooneshwa, tatizo la uhaba wa chakula nchini litapungua, kama siyo
kumalizika kabisa.
Waziri Mkuu
Mhe Kassim Majaliwa, ameahirisha Mkutano wa Pili wa Bunge mpaka tarehe
19 mwezi April 2016 saa 3 Asubuhi
likaporejea katika Mkutano wa kujadili Bajeti ya Mwaka wa Fedha
2016/2017.
Pata Picha, Habari za Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari kwa WhatsApp +255789925630 or +255756830214.
|
No comments:
Post a Comment