AHADI YA RAIS MAGUFULI:- Wizara ya Fedha yaipatia Idara ya Mahakama Sh bilioni 12.3 kuboresha Utendaji Kazi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, February 08, 2016

AHADI YA RAIS MAGUFULI:- Wizara ya Fedha yaipatia Idara ya Mahakama Sh bilioni 12.3 kuboresha Utendaji Kazi.

Wizara ya Fedha na Mipango imetoa sh.bilioni 12.3 kwa ajili shughuli za mahakama ikiwa ni sehemu ya ahadi ya  Rais Dk. John Pombe Magufuli aliyoiahidi katika kilele cha maadhimisho ya  siku ya mahakama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango amesema fedha hiyo imetolewa kwa kutimiza ahadi ya Rais ya uendeshaji wa shughuli za mahakama.

Mpango amesema kuwa ahadi ya Rais ilikuwa ni ya siku tano ambazo zimetimia kwa kutoa hundi ya sh.bilioni 12.3 ambazo zitakwenda kufanya kazi iliyokusudiwa.

Amesema kuwa Wizara ya Fedha na Mipango kutokana na ahadi hiyo imefanya kuweka wazi juu ya fedha hizo kwa waandishi wa habari.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju amesema lengo ni kuongeza kasi kwa mashauri yaliyopo kuondoshwa  pamoja na waliokwepa kodi  yashughulilikiwe.

Ahadi ya Rais ilitolewa baada ya maombi ya Jaji Mkuu, Othman Chande katika maadhimisho ya  kuanza kwa mwaka wa mahakama kudai kuwa wana uhaba fedha za maendeleo  katika kuweza kuendesha shughuli za kimahakama.
Waziri wa Fedha Mipango, Philip Mpango (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusiana na kutimiza ahadi aliyoiahidi Rais  Dkt. John Pombe Josef Magufuli alipoahidi katika maadhimisho ya siku ya mahakama hapa nchini. Kulia ni Naibu waziri wa katiba na sheria, Amon Mpanju na kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.
Mtendaji mkuu wa Mahakama Hussein Kattanga (kushoto)akimshukuru Rais  Dkt. John Pombe Josef Magufuli kwa kutimiza ahadi yake aliyoiahidi siku ya maadhimisho ya siku ya mahakama. kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Dkt. Servacius Likwelile.

Pata Picha, Habari za  Siasa, Kijamii, Biashara, Muziki na Michezo na Nyingine kwa kujiunga  na Mimi Hapa...FACEBOOK .. TWITTER .. INSTAGRAM … Pia Usisite kututumia tukio la Picha/Habari  kwa WhatsApp +255789925630 Or+255756830214.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad